Advertisements

Monday, January 21, 2019

ITUNZENI MIUNDO MBINU YA MAJI ILI MUWEZE KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA' - JENERALI MSTAAFU MWAMUNYANGE

Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph (kwanza kulia) akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) jinsi maji yanavyovunwa katika Mtambo wa Ruvu Juu - Ruvu Kibaha - Pwani. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) mitambo ya mashine za maji eneo la Ruvu Juu walipofanya ziara ya kwa ajili ya kujifunza.

Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akitoa maelezo. machache.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakionyeshwa  mitambo ya mashine za maji.
Meneja wa DAWASA Kibaha - Pwani, Crossman Makere akitoa ripoti mbele ya Wakurugenzi Bosi ya DAWASA mara baada ya kutembelea ofisini hapo.
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange.
Msimamizi wa Mradi wa Kisarawe na Kibaha injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kufika eneo la Minarani Kisarawe, Pwani kujionea ujenzi wa tanki la maji.
Mafundi wakiendelea na kazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Mwamunyange akiwa na Wajumbe wa Bodi wakitoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali yahusuyo miradi hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kujifunza wanavyofanyakazi. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Wananchi wametakiwa kutunza miradi na miundo mbinu ya maji ili iweze kuwahudumia na waondokane na tatizo la ukosefu wa maji. Akizungumza baada ya kumaliza siku ya kwanza Jenerali Mstaafu Mwamunyange amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kuwapatia maji safi na salama. "Niwaombe wananchi watunze miundo mbinu ya maji maana ujenzi wake ni gharama sana tofauti na wao wanavyofikiria wanapoona maji yamewafia majumba," amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange. Ziara hiyo ilianzia katika chanzo cha maji cha Mto Ruvu Juu, Ofisi ya DAWASA ya Kibaha, Tenki la Kibamba lenye ujazo wa lita Milioni 10 na ujenzi wa tanki la Kisarawe lenye ujazo wa Lita Milioni sita. Katika ziara yake Mwamunyage ametembelea pia Ujenzi wa mradi wa bomba la maji kutoka Kibamba (Bomba kuu la kusafirisha maji kutoka Ruvu juu) hadi Kisarawe utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha maji Lita Milioni 4 kwa siku na wananchi mbalimbali wa maeneo ya Kisarawe watafaidika na maji. Amesema kuwa, ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa tenki hilo na kama wakandarasi wataendelea hivyo kufikia mwezi Septemba mwaka huu ujenzi utakua umekamilika. Katika mradi huo Jenerali Mstaafu Mwamunyange ametembelea tenki la maji lenye ukubwa wa lita milioni 10 kwenye eneo la Kibamba na kuoneshwa pampu nne za kusukumia maji hadi Kisarawe. Kazi zingine zinazoendelea kutekelezwa na Mamlaka hiyo kwenye mradi wa Kisarawe ni ujenzi wa bomba la kusafirishia maji lenye kipenyo cha inchi 16 urefu wa Km 15.65, mabomba ya kusafirisha na kusambaza maji kwenda kwenye maeneo ya Viwanda lenye urefu wa Km 5.15 na kipenyo cha inchi 12 na lingine likiwa ni urefu wa Km 8 na kipenyo cha inchi 8.9 Ujenzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza maji lenye ukubwa wa Lita milioni 6 katika eneo la Mnarani Kisarawe na ujenzi wa Kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba. Maeneo yatakayofaidika na mradi huo ni kata ya Kisarawe, Kata ya Kazimzumbwi pamoja na maeneo ya Kiluvya, Kisopwa, Mloganzila na maeneo maalumu ya viwanda.

No comments: