ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 30, 2019

LEO NI MIAKA 9 TANGIA KUANZISHWA KWA BLOG VIJIMAMBO

Image result for VIJIMAMBO: LEO JAN 31, 2012 NI MIAKA 2 TANGU VIJIMAMBO
Hii ndiyo iliyokua picha ya kwanza kwenye blog ya Vijimambo ikionyesha timu ya Stars United ilipokua Boston, Massachusetts kwa mechi ya kirafiki na wenyeji wao.
Image result for VIJIMAMBO: LEO JAN 31, 2012 NI MIAKA 2 TANGU VIJIMAMBO
Uzinduzi wa Blog ya Vijimambo na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar Octoba 23, 2010 katika ukumbi wa Mirage.
Image result for VIJIMAMBO: LEO JAN 31, 2012 NI MIAKA 2 TANGU VIJIMAMBO
Miaka 2 ya Vijimambo.
Image result for VIJIMAMBO: LEO JAN 31, 2012 NI MIAKA 2 TANGU VIJIMAMBO
Miaka mitatu ya Vijimambo na tamasha la Kiswahili mgeni rasmi alikua Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Image result for VIJIMAMBO: LEO JAN 31, 2012 NI MIAKA 2 TANGU VIJIMAMBO
Miaka minne ya Vijimambo mgeni rasmi akiwa Waziri wa Utalii Mhe Lazaro Nyalandu(kati) kushoto ni aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula

Timu ya VIJIMBO haiamini leo January 31, 2019 Blog yako pendwa imefikisha miaka 9, tangu ilipoanzishwa January 31, 2010.

Kabla ya yote ni kumshukuruMwenyezi Mungu mwingi wa rehema kutujalia hekima, nguvu na ujasiri ikiwemo maarifa bila kuchoka kwa miaka 9 ya kuendeleza libeneke la VIJIMAMBO, Blog nyingi zimejaribu na nyingi zimeishia katikati huku nyingine zikipungua umaarufu wake.

Nimshukuru Mke wangu na watoto kwa kukubali kuchukua muda wao katika kuniruhusu kuendeleza Libeneke, asante kwa sapoti yenu najua wakati mwingine si rahisi kuchanganya Libeneke na familia lakini nashukuru kwa uvumilivu wenu na kuniunga mkono kwa hili.


Wadau wote wa Vijimambo Duniani shukurani sana bila nyinyi leo tusingefika hapa tulipo. WanaDMV kwa kuamini Vijimambo nabii hakubaliki nyumbani lakini nyie mliikubali Vijimambo na kuitumia  kwa kuwekahabari na picha zenu picha zenu na kuwaaminisha na wadau wengiine Marekani nasehemu nyingine Duniani.

Asante Ikulu na  Wizara mbalimbali nchini Tanzania kwa kuitumia Blog yenu pendwa

Shukurani Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa kuiamini Blog ya Vijimambo na timu yake kwamba ni libeneke la uhakika katika mawasiliano.

Ni jambo la kujivunia na kumshukuru Mungu Libeneke likiendelea mpaka leo kwa nguvu zote. Shukurani za pekee kwa mwakilishi wa Vijimambo Tanzania Geofrey Adroph anayepiga libeneke bila kuchoka shukurani sana kwako. NY Ebra shukurani nyingi sana na heshima kubwa kwako kwani unawakilisha vyema sana kanda za huko Newy York na majimbo ya jirani. Pongezi zingine kwa mwakilishi wa Vijimambo Dallas, Texas shukurani sana Bro kwa kazi nzuri na picha zilizoenda shule, shukurani nyingi sana kwa Cassius Mpambamaji mwakilishi wa Vijimambo Houston, Texas nakushukuru sana bro kwa kazi yako nzuri.Rachel Atlanta nani kama wewe shukrani mno mwakilishi wa Vijimambo ATL.

Shukurani zingine kwa mshirika wa Vijimambo Mubelwa Bandio na Kilimanjaro studio, Iska Jojo Vijiambo bila wewe tusingekua tunaandika haya leo.

The one and Oly Jojo fundi mitambo wa Blog ya vijimambo shukurani sana kwako. Kaley Pandukizi heshima kwako Bro kwa kuonyesha njia ya mawasiliano ya Blog ya Vijimambo. Shukurani za pekee kwa mwakilishi wa Vijimambo  katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani asante sana.

Shukurani za kipekee kwa Blogger na wanahabari wanaowezesha kutuma habari zao na kutoa ushirikiano na Blog ya Vijimambo, asante DICOTA kwa kuiaminiVijimambo, asante Ubalozi wa Marekani Tanzania na taasisi mbalimbali kwa kutitumia Vijimambo katika kuhabarisha umma.

Asante TDC Global kwa kuimamini Vijimambo tuupo na tutaendelea kuwepo.

Shukurani kwa Jumuiya za waTanzania Duniani kwa kuiamini Blog ya Vijimambo.

Timu ya Vijimambo haina kubwa litakalo walipa litakalo lingana na hayo makubwa mnayoifanyia Blog ya Vijimambo, tunaomba tuziki kushirikiana kwa kila jambo tuzidi kuendeleza LIBENEKE na kunako majaliwa tusherehekee zaidi na zaidi Besidei nyingi zaidi..

No comments: