ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 25, 2019

NAIBU WAZIRI MABULA AKERWA WADAIWA SUGU KODI YA ARDHI KUTOFIKISHWA MAHAKAMANI

 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Paul Sweya na Mkuu wa Idara ya Ardhi  Anderson Mwamengo alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa alipokutana na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya hiyo wakati wa ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma.
 Baadhi ya watendaji katika wilaya ya Kongwa wakiwepo wale wa sekta ya ardhi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua Majalada ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Kongwa alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo baada ya kukagua masijala ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Kongwa alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma. Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Paul Sweya na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Kati Ezekiel Kitlya.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi akimuongoza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kuelekea Masijala ya Ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Kongwa alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omar Nkullo.

Na Munir Shemweta, DODOMA
NaibuWaziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula ameshangazwa na halmashauri za wilaya ya Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma kushindwa kuwafikisha katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi pamoja na baadhi yao kupelekewa ilani za madai.

Dk Mabula ameziagiza halmashauri hizo mbili kuhakikisha zinawafikisha wadaiwa hao katika Mabaraza ya Ardhi kwa hatua zaidi ambapo alielezea kuwa huko maamuzi yake ni mawili ambapo mdaiwa anatakiwa kulipa ama kunyanganywa miliki yake kufidia deni.

Naibu Waziri wa Ardhi alitoa agizo hilo jana alipozitembelea wilaya hizo mbili ikiwa ni mfululilzo wa ziara zake kutembelea halmashauri mbalimbali kwa nia ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, halmashauri hizo zina wamiliki wengi wa viwanja wasiolipia kodi ya ardhi na hivyo kuzifanya kudai kiasi kikubwa cha fedha lakini idara za ardhi zinashindwa kuwachukulia hatua jambo linaloikosesha serikali mapapto.

Naibu Waziri wa Ardhi alisema, halmashauri ya wilaya ya Kongwa inadai jumla ya shilingi milioni 152 kutoka kwa wamiliki wasiolipa kodi huku ile ya Mpwapwa ikidai milioni 128,013,696.90.

Afisa Ardhi Msaidizi wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Anjelina Ndemera alisema halmashauri yake pamoja na kuwa na madeni kutoka kwa wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi lakini haikuweza kutoa ilani za madai kwa wadaiwa hao.

Kwa upande wa wilaya ya Mpwapwa, Mkuu wake wa Idara Anderson Mwamengo alisema halmashauri hiyo ina wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi mia tatu na thelathini  ambao wameandikiwa na kukabidhiwa ilani hizo.

Dkt Mabula alisema, pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuhimiza suala la kulipa kodi na Wizara ya Ardhi kujitahidi kusaidia suala hilo lakini halmashauri hazifanyi jitihada zozote katika kukusanya maduhuli ya Serikali kupitia kodi ya ardhi.

‘’Kila siku inaelezwa pelekeni ilani za madai ya kodi ya ardhi kwa wamiliki lakini hakuna ufuatiliaji wowote unaofanywa na watendaji wa sekta ya ardhi jambo linalorudisha nyuma jitihada za serikali ya awamu ya tano kukusanya maduhuli ya serikali.

Naibu Waziri wa Ardhi aliziagiza halmashauri hizo mbili kufikia tarehe 31 Machi 2019 watendaji wake wa sekta ya ardhi wawe wamewafikisha katika Baraza la Ardhi wadaiwa wote waliopelekewa ilani za madai.


Aidha, Dkt Mabula ameitaka idara ya ardhi kuhakikisha orodha ya wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi waliopewa ilani za madai inafikishwa katika kila kikao cha kamati ya Uchumi na Mazingira vya kila robo mwaka ya Baraza la Madiwani katika kila halmashauri lengo likiwa kuitaka kamati husika kuelewa suala hilo na kufanya ufuatiliaji.

No comments: