Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Tabora wakiwa katika maandamano ya kuunga mkono kampeni za upandaji miti na utunzaji mazingira jana.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi akitoa maoni yake jana wakati wa kampeni za uzinduzi wa upandaji miti kwa mkoa wa Tabora kwa mwaka huu.
Askofu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Magharibi Kati Isaac Laiser akitoa maoni yake jana wakati wa kampeni za uzinduzi wa upandaji miti kwa mkoa wa Tabora kwa mwaka huu
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua kampeni rasmi za upandaji miti mkoani humo kwaka huu.
Askofu wa Kanisa la Anglican Tabora Dkt. Elias Chakupewa akipanda mti kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora jana
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti mkoani Tabora wakisikiliza jana hotuba za viongozi mbalimbali.
Meneja wa Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania Kaznda ya Magharibi Valentine Msusa akieleza jana uharibifu ambao umeanza kufanywa katika mistu ya hifadha.
Wanakwaya wa chuo cha Ualimu Tabora wakiimba wimbo maalumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti mkoani Tabora jana.
NA TIGANYA VINCENT
TAMKO lilitolewa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kuruhusu baadhi ya vijiji na vitongoji vilivyopo katika maeneo ya hifadhi vitambulike rasmi limetafasiri vibaya mkoani Tabora na baadhi ya wananchi kwa kuanza kuvamia na kulima na kuchunga mifugo katika maeneo ya Hifadhi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania Kanda ya Magharibi Valentitne Msusa wakati uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Mkoa wa Tabora yenye la kuhifadhi mazingira ya kuifanya Tabora kuwa ya kijani. Alisema kuanzia wiki iliyopita makundi ya yameingia kutoka mkoa wa Singida na kuvamilia mistu ya Uyui, Igombe Mkuu na Mistu ya Fila na wengine wameingia na kuanza kuandaa mashamba mapya kwa ajili ya kilimo.
Msusa alisema kuwa Rais hakuelekeza watu waingie katika maeneo ya Hifadhi ya kufyeka miti na kusema kinachoendelea ni kitendo kinachokiuka maelekezo ya Rais kwa kuwa hakusema watu wakaanzishe mashamba mapya ya ndani ya Hifadhi. “Jamii nawaomba acheni kuingia katika Hifadhi ya kuanzisha mashamba mapya hayo sio maelekezo ya Mheshimiwa Rais … kwani vitendo hivyo vinahatarisha chanzo cha maji ya Mkoa wa Tabora”alisema.
Alisema watu watakaokutwa ndani ya hifadhi wakianzisha mashamba mapya na kuendesha shughuli za ufugaji watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa wanakiuka maelekezo ya Rais na Sheria. Meneja huyo wa Kanda ya Magharibi wa TFS aliwataka watu wote ambao walishaondolewa siku za nyuma katika maeneo ya Hifadhi wasidiriki kurudi kwani watachukuliwa hatua.
Msusa aliitaka jamii kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanalinda na kuhifadhi maeneo yote ya Hifadhi za Mistu ili yasivamiwe na watu na kuendesha uharibifu. Aidha alisema TFS inatarajia kupanda miti katika maeneo yote ya Hifadhi ambayo uharibifu ulifanyika ikikwemo katika Wilaya ya Nzega kama mkakati wa kuhifadhi na kutunza mazingira.
Awali viongozi wa dini Mkoani Tabora wameitaka jamii kuunga mkono juhudi za Serikali za upandaji na utunzaji miti kwa ni muhimu katika ujenzi wa uchumi wa kati kuelekea ujenzi wa viwanda nchini. Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Magharibi Kati Isaac Laiser alisema kuwa upandaji wa miti ni jukumu la kila mtu na mtu anayekataa kupanda miti hamgomei Mkuu wa Mkoa bali anaigomea Serikali.
Aliongeza kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ujenzi wa kati kuelekea ujenzi wa viwanda na utunzaji wa mazingira na kuongeza kuwa vitu vina uhusiano mkubwa. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi alisema jambo la uhifadhi wa mazingira wananchi wote kwa kuwa ni maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwa aliumba ili wanadamu wayatunze na kuyahifadhi mazingira.
Alisema suala la upandaji miti halina dini , kabila, siasa kwa kuwa miti ni muhimu kwa watu wote. Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwaagiza viongozi kuanzia ngazi za Vitongoji hadi Mkoa kusimamia zoezi la upandaji kiti katika maeneo yao na kiongozi atakayeshindwa kutekeleza jukumu hilo atakuwa haina sifa ya kuwa kiongozi.
No comments:
Post a Comment