ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 17, 2019

Dkt. Gwajima Atua Dar na Kampeni ‘Coordination’


 Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Dorothy Gwajima, akiwa katika picha ya Pamoja na Muunguzi Sarah John na watumishi wengine wa Zahanati ya Malambamawili, mkoani Dar-es-salaam wakati wa ziara hiyo.
 Dkt. Doroth Gwajima, alipowasili katika  hicho  Zahanati hiyo ya Malambamawili, akisaini kitabu cha wageni huku, watumishi wakiwa wamesimama nyuma yake kabla yakuanza ziara kwenye kituo hicho na kufanya hamasa ya huduma za Afya.
Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza jambo  wakati wa ziara yake mikoani, akihimiza masuala yakufanya kazi kama timu ili kupata tija katika utendaji.  


Na. Atley Kuni- OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Dorothy Gwajima, amefanya ziara mkoani Dar-Es-Salaam huku akiendeleza kampeni yake ya kufanya kazi kwa ushirikiano aliyoianza mkoani Dodoma kwakuwataka watendaji serikali kutambua na kuheshimu ubunifu wa mtumishi mmoja mmoja.

“Viongozi wote ngazi zote tuzidi kuungana kutambua juhudi za kila mtumishi na hasa junior Staff, kwani ipo siri kubwa katika nguvu ya kutambua na kupongeza amabapo hata changamoto zitageuka kuwa fursa” alisema Gwajima

Gwajima alisema kuwa, mapungufu na uhaba vitageuka kuwa fursa kwakua macho na akili ya ndani vitafunguka na kukabiliana na hayo yote na kupata ufumbuzi wa matatizo mbalimbali katika sehemu za kazi wanapo watia moyo watumishi.

Katika ziara yake ya kwanza, aliyoifanya mkoani Dodoma Dkt.Gajima alikutana na Sekretarieti ya mkoa huo chini ya katibu Tawala wa Mkoa na hatimaye kufanya kikaokazi na Kamati ya Afya ya Mkoa, ambapo katika vikao vyote viwili alihimiza utendaji kazi wa pamoja (coordination, Harmonization, Involvement and Motivation)

Katika ziara hiyo ya Mkoa wa Dar-Es-Salaam, alipongeza jitihada za mtumishi Muuguzi Sarah John wa Zahanati ya Malambamawili Kata ya Msigani, Manispaa Ubungo kwa jitihada zake alizo onesha katika utendaji uliotukuka hasa katika kuhamasisha watu kwenda kwenye huduma za afya.

Dkt. Gwajima. Alisema, Muunguzi Sarah John katika Zahanati hiyo amekuwa chachu yakuhamasisha wateja wao kwa kuwatungia nyimbo, kuimba na kucheza nao hali iliyo pelekea watu katika Kata hiyo kumpenda kwa uwezo wake huo wakuhamasisha na kuwafanya watu wengi kuhudhuria katika huduma za afya kwenye kituo hicho kilicho anzishwa Julai, 2018 ndani ya kata hiyo.

“Siyo Rahisi kwa Muuguzi kujishusha hadi kucheza na wateja wake, inahitaji Moyo wa kupenda kazi, kulipenda taifa na uzalendo wa hali ya juu kutoka Moyoni” alisema Gwajima.

Bi. Sarah amekuwa akienda sambamba na Kauli mbiu ya Mhe. Rais yakutaka kila mtu azae bila kupangiwa idadi ya watoto, ila wazingatie malezi kwa wototo atakao wazaa kwa kuwapatia huduma za msingi.

Hii imekuwa ni ziara yake ya pili tokea Dkt. Gwajima, ateuliwe na Mhe. Rais kushika wadhfa Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya) ambapo katika ziara hiyo, waliungana na uongozi wa Kata ya Msigani na wananchi na watendaji kisha kufanya hamasa ya watu kushiriki katika huduma za afya msingi huku rai yake kubwa akiilekeza kwenye kufanya kazi kama timu moja ili kufikia maendeleo endelevu kwa watu kuwa na afya njema.

No comments: