Kundi la Mkubwa na Wanawe wakishambulia jukwaa katika onesho lao la jana usiku 7 Februari 2019, kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar |
NA ANDREW
CHALE, ZANZIBAR
KUNDI la
wanamuziki wanaokuzwa la Mkubwa na Wanawe usiku wa 7 Februari 2019 limeweza kukonga nyoyo za watu waliojitokeza
kushuhudia tamasha la 16 la Kimataifa la Sauti za Busara, kwenye viunga vya
Ngome Kongwe, Unguja.
Kundi hilo
limeweza kuonesha umahri wao wa kuimba na kucheza jukwaani huku wakiendana
sambamba na mapigo na ala za muziki wa bendi ‘live’, iliamsha shangwe za mara
kwa mara kwa mashabiki waliofurika Ngome
Kongwe.
Vijana hao
wa waliweza kuimba nyimbo zaidi ya tano (5)
ikiwemo ya Stata ukiimbwa na
mwanadada Catrima Wegesa huku nyimbo
zingine zikiimbwa na wasanii wengine Abdala Mustapha ‘Kisamaki’ huku kijana
mdogo kabisa wa kundi hilo Abdul Kadry akiwa kivutio kila alipopanda kuimba
kweney jukwaa hilo la Busara.
Dogo Kadry
aliweza kuimba nyimbo zaidi ya mbili ikiwemo kuurudia wimbo wa Asu ulioimbwa na
Abdul Misambano.
Aidha,
Wasanii pia waliweza kuimba nyimbo za wasanii waliowahi kupitia kundi hilo
zikiwemo za ‘Mototo wa udongo’ na ‘Watakubali’.
Kundi hilo lililo chini ya muasisi wake, Said
Fella ‘Mkubwa Fella’ ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kilungule ya wilayani
Temeke, Dar es Salaam hadi sasa lina vijana wanaofanya kazi za Sanaa za Muziki
zaidi ya 100.
Miongoni wa
wasanii waliowahi kuwa kwenye kundi hilo na kwa sasa wanajitegemea ni pamoja na
Dogo Aslay, Mboso na wengine wengineo.
Miaka miaka
kadhaa iliyopita wasanii hao Dogo Aslay na Mboso waliwahi kushiriki tamasha
hilo huku wakiwa vijana wenye umri mdogo
ambapo walikuwa kivutio kama ilivyo kwa sasa kwa msanii mpya wa kundi hilo Dogo Kadry.
Mpaka Mkubwa
na Wanawake Crew wameshatoa nyimbo mbalimbali zikiwemo : Tofauti, 2012;
Nawashusha Down, 2013; Fanya Yako, 2014; Unanitusi, 2015; Sitakitararira, 2016;
Naelewa, 2016; Yerere, 2016
No comments:
Post a Comment