Timu ya Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mkoa wa Njombe (waliokaa watatu upande kulia) wakitoa huduma kisaikolojia na kijamii kwa Familia ya Bw. Danford Nziku iliyopoteza watoto watatu kutokana na vitendo vya utekeaji na mauaji ya Watoto vilivyotokea mkoani Njombe. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Wananchi mkoani Njombe wameishauri Serikali kutoa elimu kwa wananchi juu ya Kaya kuzingatia kukaa karibu ili kuongeza usalama na kuepuka vitendo vya utekaji na mauaji ya Watoto na vitendo vyote vya kihalifu.
Ushauri huo umetolewa leo wakati Timu ya Wataalam wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mkoa wa Njombe walipoitembelea familia zilizopoteza watoto kutoka na vitendo vya utekaji na mauaji ya watoto kwa lengo la kutoa pole na kutoa msaada wa huduma za kisaikolojia na kijamii. .
Wakiwa katika Familia ya Bw. Dau Ng'aala ya Kambarage Halmashauri ya Mji wa Njombe Wilayani Njombe iliyopoteza Mtoto wao Oliver Ng'aala(5) aliyepotea Desemba 07/2019 na kupatikana Desemba 08 akiwa amefariki.
Familia hiyo imesema kuwa suala la kaya kukaa mbali mbali imekuwa ni suala mbalo kwa sasa linatakiwa kufanyiwa kazi kwani kukaa karibu kunaongeza usalama kwao.
Bw. Dau Ng'aala ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Njombe kwa kuwekea mkazo katika uchunguzi wa matukio ya utekeaji na mauji ya watoto kwani yamesababisha huzuni kubwa kwa familia mkoa wa Njombe na taifa kwa ujumla.
Ameongeza kuwa wao kama familia watatoa ushirikiano kwa vyombo vyote vya mamlaka katika kuhakikisha watuhumiwa wafikishwa katika sehemu husika na Sheria inafuata mkondo wake kwa wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya kinyama.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bi. Teresa Yomo ameihakikishia ushirikiano familia ya Bw. Dau Ng'aala na familia zote zilizopatawa na matatizo kuwwa atahakikisha wanapata msaada wa huduma za kisaikolojia na kijamii ili kurudi katika hali ya kawaida.
“Tupo pamoja na tutahakikisha mnapata msaada wa kisaikolojia na kijamii kwani utawasaidia mrudi katika hali yenu ya kawaida kama zamani” alisema
Kwa upande wake Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu amesisitiza umoja na mshikamano katika familia wakati huu huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku za uzalishaji mali.
No comments:
Post a Comment