Advertisements

Monday, March 25, 2019

Kampuni ya usafirishaji ya LITTLE yatinga Dar

 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Usafirishaji ya LITTLE, AshishKukre ti (katikati), Mjumbe wa Bodi, Abaas Mfundo (kushoto), na Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Jefferson Aluda, wakikata keki wakati wa uzinduzi wa huduma za kampuni  hiyo Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Usafirishaji ya LITTLE, Ashish Kukreti akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma za kampuni hiyo Tanzania katika hafla iliyofanyika JIjini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Meneja Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya Little, Ashish Kukreti akizungumza na baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi wa huduma za kampuni ya usafirishaji  ya LITTLE jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa LITTLE Jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya usafirishaji abiria kupitia mtandaoni ijulikanayo kama LITTLE imezindua huduma zake Tanzania zenye lengo la kuchnagia katika kuleta suluhu katika adha ya usafiri.

Huduma hii itapatikana kwa njia ya mtandao na kuwakutanisha madereva na wasafiri kupitia zao simu ya kiganjani.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hizo jijini Dar es salaam katika hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mkuu wa LITTLE Ashish Kukreti amesema kwamba huduma hizo zinalenga kusaidia kurahisisha huduma ya usafiri katika jiji la Dar es salaam

“Kutokana na mahitaji na umuhimu mkubwa wa usafiri katika jiji la Dar es salaam, napenda kuzindua huduma hii ambayo itakuwa msaada mkubwa katika kurahisisha usafiri katika jiji la Da res sama” alisema

Alisema huduma za LITTLE ni za haraka na uhakika ambapo mtumiaji wa simu ya mkononi itamlazimu kubonyeza kitufe na kuita usafiri wa aina yoyote kutoka kwa dereva atakayekuwa amejiunga na huduma za LITTLE

“Tayari tumeshatoa mafunzo na kusajili madereva takriban 500 ambao tayari wanafahamu matumizi ya huduma zetu na tunatarajia kutoa mafunzo zaidi kwa wasafiri na madereva ili huduma yetu iwafikie watu wengi zaidi” alisema

LTTLE ni kampuni ya kimataifa ambayo ilianzishwa mwaka 2016 na sasa hivi imefungua shughuli zake katika nchi za Uganda, Kenya, Zambia na sasa Tanzania. Kukreti anasema wanataka kutatua changamoto za usafiri katika jiji la Dar es salaam na kutoa ajira kwenye jamii.

Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani nan je ya sekta ya usafirishaji.

No comments: