Viongozi wa Serikali, Siasa na Wananchi wakimsalia Mwakilishi wa zamani wa Jimbo la Mkwajuni Marehemu Mbarouk Wadi Mtando aliyefariki Hospitali ya Muhimbili Dar na kuzikwa Kijijini kwao Mkwajuni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiteta na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulidi wakatiu wa mazishi ya Mwakilishi wa Zamani wa Jimbo la Mkwajuni Mbarouk Wadi Mtando Kijijini kwao Mkwajuni Mkoa Kaskazini Unguja. Wa Tatu Kushoto ya Balozi ni Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dr. Juma Abdullah Saadala { Mabodi }.
Harakati za mazishi zikiendelea kwenye Viunga vya Kijiji cha Mkwajuni kuuhifadhi Mwili wa Mwakilishi wa zamani wa Jimbo la Mkwajuni Marehemu Mtando kwenye malazi yake ya kudumu.
Spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akimwaga dongo kwenye Kaburi alilozikwa Mwakilishi wa zamani wa Jimbo la Mkwajuni Marehemu Mbarouk Wadi Mtando.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akiifariji Familia ya Mwakilishi wa zamani wa Jimbo la Mkwajuni
Marehemu Mbarouk Wadi Mtando mara baada ya mazishi yake Kijijini kwao
Mkwajuni.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Mamia ya Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Kisiwa cha Unguja Mjini
na Vijijini leo wamehudhuria mazishi ya Mwakilishi wa zamani wa Baraza
la Wawakilishi Zanzibar Marehemu Mbarouk Wadi Mtando yaliyofanyika
kijijini kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Marehemu Mtando aliyewahi kuwa Mwakilishi wa lililokuwa Jimbo la
Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini “A”katika kipindi cha Mwaka 2005 hadi
2010 alifariki Dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbiji Mjini Da
es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mazishi hayo yaliongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi akiambatana pamoja Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Zubeir Ali Maulidi, Spika Mstaafu Pandu Ameir
Kificho, Naibu Katibu wa CCM Zanzibar Dr. Juma Abdullah Saadala
{Mabodi}, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Viongozi Waandamizi wa Serikali
pamoja na wale wa Vyama vya Kisiasa.
Marehemu Mbarouk Wadi Mtando ambae alikuwa akisumbuliwa na Maradhi ya
Kisukari kwa kipindi kirefu amewahi kupatiwa matibabu Nchini India,
akianzia tiba ya Maradhi yake katika Hospitali mbali mbali hapa
Nchini.
Kama ilivyo kawaida ya mazingira ya Watoto wa Kitanzania Marehemu
Mbarouk Wadi Mtando alipata mafunzo ya Elimu ya Dini na Dunia Kijiji
kwao Mwajuni na baadae kujishughulisha na mambo ya Kibiashara na
hatimae masuala ya Kisiasa yaliyompelekea kuwa Mwakilishi wa Jimbo la
Mkwajuni kwa kipindi kimoja.
Jamii itaendelea kumkumbuka Mwakilishi huyo wa zamani wa Jimbo la
Mkwajuni kutokana na ukarimu wake kwa Jamii uliompelekea kuwa Maarufu
kutokana na moyo wake wa kisaidia bila ya kujali Rangi, Umri, Dini au
Itikadi za Kisiasa.
Marehemu Mbarouk Wadi Mtando ametangulia mbele ya Haki baada ya kuitwa
na Mwenyezi Mungu Subuhanahu - Wataalah kama walivyoitwa
waliomtangulia na kuacha Wamilia ya Watoto kadhaa.
Mwenyezi Muungu ailaze roho ya Marehemu Mbarouk Wadi Mtando mahali
pema peponi. Amin.
No comments:
Post a Comment