Dar es Salaam. MAPENZI ni kitu kigumu kukitafsiri kwa kuona picha kwa mtu, isipokuwa wapendanao ndio wanaweza wakaeleza kinaga ubaga namna wanavyoyafurahia kupendana kwao, hilo ndilo lililowafanya wahenga kusema kipenda roho hula nyama mbichi.
Upana wa mapenzi ndio ulioibua msemo mwingine wa hakuna mkate mgumu mbele ya chai, ukitaka kuamini hilo muulize mke wa beki mahiri wa Yanga, Kelvin Yondan anayejulikana kwa jina la Nance Mussa ingawa anapenda kuitwa Nance Yondan.
Ni nadra kumwona Yondan anatabasamu, akizungumza ovyo kama ilivyo kwa
wachezaji wengine ambao ni wacheshi, pamoja na mwonekano huo mbele ya wadau wa soka ila kwa mke wake anaonyesha tabasamu kama lote na sura yake ya ukauzu inakuwa mwisho getini anapoingia nyumbani kwake. Mwanaspoti limefanya mahojiano na mke wa Yondan, kujua anapokuwa nyumbani ni mume wa aina gani kwake? Pia kujua mchango anaompa mume wake katika kazi yake ya soka.Upana wa mapenzi ndio ulioibua msemo mwingine wa hakuna mkate mgumu mbele ya chai, ukitaka kuamini hilo muulize mke wa beki mahiri wa Yanga, Kelvin Yondan anayejulikana kwa jina la Nance Mussa ingawa anapenda kuitwa Nance Yondan.
Ni nadra kumwona Yondan anatabasamu, akizungumza ovyo kama ilivyo kwa
Nance anasema kama kuna kitu hawakijui wadau wa soka nchini kuhusu mume wake, Yondan ni ukarimu, tabasamu lisilo na kelele ambalo limejaa vitendo zaidi, hapendi kuonea mtu wala kuonewa na ni mchapakazi.
Anafichua Yondan, hapendelei sehemu za watu wengi ama kelele anapokuwa mapumziko na kudai anapendelea kukaa kwa muda mrefu na familia yake, huku muda wote akiwa mwenye furaha na kupenda kucheza na watoto wake.
“Pamoja na watu kumwona mume wangu ni mtu wa hasira muda wote au mgomvi anapokuwa nyumbani mambo hayo yanaishia getini, akiingia ndani anakuwa na tabasamu la kufurahia kutuona, huku akiniita muda wote mpenzi ama mama watoto wake.
“Ni baba mwema, mstaarabu, mwenye upendo na sisi ila asichokipenda ni mkusanyiko wa watu wengi na ndio maana tunaishi sehemu tulivu sana yaani sio changanyikeni, hata akitaka tutoke anatafuta maeneo ya utulivu ili tukiongea tuwe tunasikilizana,” anasema.
MCHANGO WAKE
KATIKA SOKA
Anasema ana mchango mkubwa kuhakikisha mume wake anakuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, akitaja mambo matatu muhimu anayoyafanya kwa Yondan kuwa ni kulinda kazi yake, kuwa karibu naye kwa kila hatua na kumkosoa anapofanya vibaya.
Anasema Yondan akiwa na mechi hata akitokea kwake, huwa hamruhusu kumpa unyumba badala yake anakuwa anamhimiza kufanya mazoezi na kuhakikisha anakuwa fiti kwa ajili ya kazi inayokuwa mbele yake.
“Huwa nafuatilia ratiba yake ya mechi, lengo ni kuhakikisha namjengea mudi ya kufanya kazi kwa moyo, sio kila mechi wanakuwa kambini zingine wanatokea nyumbani, akiwa nyumbani basi huwa namlinda kuhakikisha baadhi ya mambo tunajizuia kuyafanya. “Hata akiniambia mke wangu ninahitaji leo tufanye hivi, namkumbusha na kumwambia mume wangu vumilia mbele una majukumu ya mechi na hiyo kazi ndio inakufanya ututunze na tuishi kwa kupata mahitaji muhimu.
“Huwa ni mwelewa na huwa anashukuru anapoona namkumbusha juu ya majukumu yake, siishii hapo tu bali huwa naenda mbali kwa kumpa kampani ya mazoezi anayoyafanya kila siku, anapata moyo na kujituma ili kazi yake kuwa bora kila anapopewa nafasi ya kucheza na kocha wake,” anasema.
Pia anasema Yondan sio mtu wa mambo mengi anapokuwa nje ya kazi yake, jambo analoliamini linamsaidia kudumu kwenye kiwango chake, ikiwemo yeye mwenyewe kumlinda kubaki kwenye misingi ya soka.
Mbali na hilo amefunguka na kuweka wazi anapenda mume wake anapokuwa anamwona ana juhudi ya kazi yake, akiwa amecheza chini ya kiwango anamkalisha chini na kumwambia ukweli ili kama kuna tatizo aweze kulirekebisha kabla halijaota mizizi.
“Sipendi kumwona Yondan anacheza chini ya kiwango, ikitokea kafanya hivyo, natafuta namna nzuri ambayo hatutakwazana namweleza na huwa napenda kujua sababu iliofanya kazi yake iwe mbaya kwa siku hiyo, huwa anaumia sana nikimwambia hivyo.
“Akifanya vizuri pia namwambia mume wangu leo umefanya kazi nzuri kwani huwa naangalia kila mechi anayocheza, lengo ni kuona anakuwa mfano wa kuigwa kwa uwezo dhidi ya chipukizi ambao wanakuja nyuma yake na wakati mwingine namwandalia zawadi kabisa ya kumpa moyo,” anasema.
YONDAN ALIKATA TAMAA
Nance anafichua kuna wakati Yondan anakuwa anatamani kuachana na soka, lakini anakuwa anamtia moyo na kumwambia bado hawajafikia kwenye malengo yao, hivyo anamwaminisha huduma yake bado inahitajika kwa jamii. “Yondan hapendi kuzinguliwa, amewahi kuniambia mara kadha anaachana na soka, maneno hayo yanakuwa yananiumiza sana, ingawa anaelewa atakuwa na kitu kinachomuumiza zaidi mpaka kufikia maamuzi hayo.
“Huwa namwambia mume wangu vumilia, hakuna kazi ambayo inakosa vikwazo pia huwa namsisitiza juu ya malengo yetu bado hatujafika hivyo anatakiwa kupigania ndoto yetu, huwa ananielewa kisha anaendelea na shughuli zake kama kawaida,” anasema.
MZUKA WAKE AFCON
Anasema baada ya mume wake Yondan, kuchaguliwa kuwa mmoja wa wachezaji wa kuunda kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambacho kilienda Misri kwa ajili ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika ‘AFCON’, alimwambia neno moja wasiende kushiriki bali wakalipambanie taifa la Tanzania dhidi ya wapinzani wao.
“Kwanza nilimpa hongera kwa kuaminiwa na kocha wake, Emmanuel Amunike na Watanzania kwa jumla, nikamwambia akajitume kwa ajili ya kutetea taifa lake kwa maana ya kuonyesha juhudi zake binafsi na kushirikiana na wenzake.
“Huwa sipendi kusikia mtu anapofanya kitu cha ushindani halafu anasema anashiriki, nimemwambia waende kupigania taifa lake na sio kushiriki kwani wanaoshindana nao wana malengo ya kutwaa ubingwa na sio kushiriki.
“Pengine wasichokijua wadau wa soka kutoka kwangu, napenda Yondan nikimwona anafanya kazi nzuri ambayo italeta heshima kwa familia, akifanya ovyo hata watoto watakosa amani mtaani kusikia baba yao anatukanwa ama mimi mwenyewe sitakuwa na furaha, neno shiriki maishani mwake sipendi kulisikia, natamani kuona anapambana,” anasema.
HASIRA ZAKE
ZINATULIZWA HIVI
Nance anasema akigundua Yondan ana hasira ametaja anamtambua kwa ishara ukimya anaokuwa nao hivyo, anakuwa karibu naye kumwambia maneno mazuri ya kumwondoa ‘stres zake’.
“Nakuwa karibu naye na kusimamisha baadhi ya ratiba za kazi zangu za nyumbani, huwa namwambia nampenda na ndiye furaha yetu yaani mimi na watoto wake, akisikia hilo huwa ni mwepesi wa kuachana na mambo yanayokuwa yanamsumbua kichwani.
“Njia nyingine nachukua watoto wake tunaanza kucheza naye, basi akikaa sawa ananiambia mke wangu kinachonisumbua ni moja mbili tatu, pia ananiambia kama kuna kitu hapendi kukiona kwangu ni mimi kununa, jambo hilo linamchefua kabisa, hivyo nakuwa najitahidi kuwa mwenye tabasamu hata akinikosea namwambia kwa amani na anarekebisha,” anasema.
ASICHOPENDA YONDAN
Nance anasema Yondan hapendi kupikiwa chakula na dada wa kazi, hivyo anaeleza huwa anamwandaliwa mwenyewe kuhakikisha anafurahia kupumzika nyumbani kwake. “Chakula anachopenda ni ugali na mlenda na pembeni kuna samaki, huwa anakifurahia sana hata akila kila siku hawezi kulalamika.
“Na sio mtu wa mitoko mara nyingi anapenda kushinda na sisi hata kama anahitaji kunywa bia mbili tatu basi ananunua na kunywea nyumbani, huyo ndiye Yondan kwa kifupi,” anasema.
VITU ANAVYOCHUKIA NANCE
Kama kuna kitu anachochukia Nance kutoka kwa Yondan ni hasira zake za uwanjani, kitu ambacho amedai bado anaendelea kuzungumza naye ili kuachana na tabia hiyo. “Kiukweli sipendi anavyochukiachukia ovyo uwanjani, huwa namwambia ukikasirika unakuwa mbaya, uzuri wake hapendi ninune, akinikuta nimenuna namwambia ulichokifanya kimeniudhi sana.
“Ninachompendea mume wangu anacheka ananiambia mama watoto sipendi furaha ikosekane nyumbani, anaomba msamaha na kuniambia sijui kinachokuwa kinatokea ndio maana anafanya vile,” anasema.
YONDAN KUVULIWA
UNAHODHA
Yondan alivuliwa unahodha na kocha wake Mwinyi Zahera na kumpa cheo hicho Ibrahim Ajibu anayedaiwa kusaini Simba, miaka miwili. Nance amezungumzia tukio hilo alishukuru Mungu baada ya Yondan kulichukulia ni tukio la kawaida na kuahidi kushirikiana na Ajibu, ambaye alikabidhiwa mikoba yake.
“Huwa namshauri kutegemeana na jinsi ambavyo anakuwa amelipokea tukio lenyewe, mfano la unahodha nikawa nimeliona kwenye mitandao ya kijamii kisha nikaanza kumpigia simu za kumpa maneno mazuri.
“Hakuniambia wakati ule ule na wala hakuonyesha kuna tukio ambalo limetokea, mpaka alipofika nyumbani ndipo akanisimulia kilichotokea tena baada ya kumuuliza.
“Akanijibu mke wangu huo ndio mpira una mambo mengi, nimechukulia kawaida sikutaka hivyo uwe na amani na tuachane na hilo tuendelee na maisha yetu ya kujenga familia, nikashindwa kuendelea ikanibidi niendeleze furaha yake anayoitaka,” anasema.
KUMTEMEA MATE KWASI
Msimu wa 2017/18 Yondan alimtemea mate mchezaji wa Simba, Mghana Asante Kwasi, walipokutana kwenye mechi ya watani wa jadi, tukio ambalo mke wake amekiri lilimuumiza na kumkwaza kabisa.
Anasema anakumbuka hiyo mechi hakufanikiwa kuitazama kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake, lakini alifanikiwa kuona tukio hilo likishika kasi kwenye mitandao ya kijamii.
“Niseme ukweli niliumia na kuishiwa nguvu, aliporudi nyumbani kama mwanamke sikutaka nikwazane naye, nikamkaribisha kwa furaha ya usoni moyoni nikiwa na hasira na tukio alilofanya.
“Baadaye tumekaa faraga nikamwambia, mume wangu kwa nini umefanya tukio la aibu na baya kiasi hicho, alinijibu kanitukania mama yangu, nilishindwa uvumilivu na nikaona kile kitendo kitatuliza hasira nilionayo lasivyo ningefanya kitu kibaya zaidi.
“Akaendelea kuniambia mke wangu, hakuna tusi linaloniuma kama mtu kunitukania mzazi ambaye hana uhusiano na kile ambacho nakifanya uwanjani, Kwasi amenikwaza kupita kiasi nilijikuta nafanya tukio, kwa kuwa sipendi kuongea wananiona mimi mbaya ila Mungu ndiye anayenijua vizuri, baada ya kuona vile nikampa pole na kumshauri wakati mwingine atumie hekima ya kunyamaza,” anasema.
WATOTO WAKE
Katika maisha yao ya ndoa Yondan, amefanikiwa kupata watoto watatu, Patrick (11), Brian (6) na Queen (3),Nance anasema wa kwanza na wapili wanapenda kucheza mpira.
“Hao wawili wa kiume wanapenda sana mpira, baba yao anawasapoti na kuwasisitiza elimu, hivyo tunamshukuru Mungu kwa baraka hizo,” anasema.
No comments:
Post a Comment