Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi na Mbunge wa Jimbo hilo Bahati Abeid Nassir wakizungumza na Wanamichezo wa Mpira wa Pete wa Timu za Wadi za Mahonda na Fujoni kabla ya kuwakabidhi vifaa vya Michezo hapo Tawi la CCM Kitope “B”.
Balozi Seif na Mbunge Bahati wakiwakabidhi Vifaa vya Michezo Viongozi wa Timu ya Mpira wa Pete ya Fujoni Mwanafatu Othman na Ramla Said.
Balozi Seif na Mbunge Bahati wakiwakabidhi Vifaa vya Michezo Viongozi wa Timu ya Mpira wa Pete ya Mahonda Zawadi Aley na Zainab Issa.
Balozi Seif akimkabidhi Kepteni wa Timu ya Mpira
wa Pete ya Mahonda Fedha za Usafiri wa wachezaji hao kwa ajili ya
kushiriki mchezo wa majaribio huko Mkokotoni Mkoa Kaskazini Unaguja.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Azma ya Uongozi wa Jimbo la Mahonda bado ipo pale pale katika
kuhakikisha inaimarisha Michezo ili ifikie siku Jimbo hilo liwe na Timu
iliyopevuka kimichezo na kushiriki Mashindano makubwa zaidi ya
Kimataifa.
Mwakilidhi wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa
hafla fupi ya kuzikabidhi Vifaa vya Michezo Timu mbili za Mpira wa
Pete {Netball} za Wadi za Mahonda na Fujoni iliyofanyika katika Ukumbi
wa Tawi la CCM Kitope “B” Wilaya ya Kaskazini B.
Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi Vifaa hivyo kukamilisha ahadi
iliyotolewa na Mke wake Mama Asha Suleiman Iddi aliyoitoa baada ya
kushuhudia pambano la kirafiki la Mchezo wa Mpira wa Pete {Netball}
uliozikutanisha Timu za Madada wa Fujoni dhidi ya Kitope lililofanyika
katika uwanja wa mahonda Kiwandani mnamo Tarehe 5 Febuari Mwaka huu wa
2019.
Alisema uimarishaji huo wa Michezo ndani ya Jimbo hilo unakwenda
sambamba na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuimarisha Sekta ya
Michezo wa vile hivi sasa mbali ya kusaidia kulinda afya lakini pia
imekuwa soko la ajira.
Balozi Seif aliwaomba Vijana wa Kike mbali ya kuendeleza mchezo wa
Pete lakini pia wana fursa ya kuandaa Timu ya Jimbo ya mpira wa soka
kwa vile tayari upo muelekeo wa kuimarika kwa mchezo huo kwa upande wa
akina mama kama hivi sasa inavyoonekana kwenye mashindano ya Dunia ya
Soka la Wanawake.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mahonda Bahati Abeid Nassir amesema inapendeza
kuona hivi sasa vijana wengi wa kike wamehamasika kushiriki kwenye
michezo mbali mbali inayoongeza ajira hasa Vikosini.
Mbunge Bahati aliwataka Wanawake hao wa timu za Mpira wa Pete wa Wadi
za Mahonda na Fujoni wafanye mazoezi kwa malengo na kuacha ile tabia
ya kuonekana Baadhi ya Wanawake hao huharibika kwenye Michezo jambo
ambalo halipendezi hata kidogo.
Aliwaahidi Vijana hao wa kike kwamba iwapo watashinda kwenye
mashindano yanayowakabili atakuwa tayari kuwaandalia safari ya
matembezi ili kubadilisha mawazo kwa vile kutembea ni kusoma.
Katika hafla hiyo Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi Seti mbili za Jezi
zilizokamilika Mipira, Viatu pamoja na Fedha za Soksi kwa Timu hizo za
Mpira wa Pete za Wadi ya Mahonda na Fujoni.
No comments:
Post a Comment