WATU saba wakiwemo wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori, uongozi wa Azam Media umethibitisha.
Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Julai 8, 2019 eneo la Shelui mkoani Singida wakati wakieleleka wilayani Chato mkoani Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi.
Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zinaeleza kuwa wafanyakazi hao walikuwa katika gari aina ya Coaster na kwamba madereva wawili wa magari hayo nao wamefariki dunia.
“Katika basi hilo dogo wafanyakazi walikuwa kumi, watano wamejeruhiwa,” zinaeleza taarifa hizo.
Uzinduzi wa hifadhi hiyo unafanyika kesho Jumanne Julai 9, 2019 na Rais wa Tanzania, John Magufuli.
Wafanyakazi wa Azam waliofariki ni:
Said Haji – Camera
Charles Wandwi – Camera
Salim Mhando – Switcher
Florance Ndibalema- Sound
Kasongo – Engineer
Majeruhi ni:
Said Mwinshehe- Camera
Masawe- Engineer
No comments:
Post a Comment