ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 12, 2019

Simba wakubali kupigwa faini CAF

By Thobias Sebastian

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), walitangaza mwisho wa usajili wa wachezaji ambao watacheza Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika mwisho ni Julia 10, na baada ya hapo kutokuwa na faini.
Timu za hapa Tanzania ambazo zinashiriki mashindano hayo Azam, KMC, Yanga na Simba wote wamepeleka orodha ya wachezaji ambao watataka kuwatumia msimu ujao.
Simba wao mbali ya kupeleka CAF, majina ya wachezaji ambao wanataka kuwatumia msimu ujao bado mchezaji mmoka ambaye jina lake halijapelekwa na wameweka wazi wapo tayari kupigwa faini.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Mulamu Ng'ambi alisema watafunga usajili baada ya kumpata mchezaji mmoja wa kigeni ambaye bado Wapo katika harakati za kumtafuta.
Ng'ambo alisema wapo tayari kupigwa faini pindi watakapo chelewa kupeleka usajili wa jina lake CAF, ambao tayari mwisho wa zoezi la usajili wa awake umesha malizika.
"Faini siyo tataizo ila tunaangaika kupata mchezaji mazuri ambaye atakuja kuongeza kitu kati timu kwenye mashindano yote ambao tutashiriki msimu ujao," alisema.
"Tutakamilisha usajili wa mchezaji huyo mmoja kabla ya zoezi la usajili wa ndani kufungwa ili kuweza kumtumia katika mashindano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo huko tumedhamilia kufanya vizuri Pia," alisema Ng'ambi.
Usajili wa ndani utafungwa mwisho wa mwezi huu Julai 31, wakati ule wa CAF, ulifungwa Julai 10, na baada ya hapo kutokuwa na faini ya Dola 250, sawa na pesa ya Kibongo zaidi ya Sh 500,000.

No comments: