ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 12, 2019

DC KASESELA ATATUA MGOGORO WA ARDHI WA FAMILIA YA MZEE MWEND

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli manispaa ya Iringa. 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli manispaa ya Iringa. 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli manispaa ya Iringa na akiwa amezungukwa na wanafamilia pamoja na mashahidi waliohudhuria kutatua mgogoro huo. 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefanikiwa kutatua mgogoro wa familia ya mzee Mwenda iliyopo katika kata ya Nduli uliodumu kwa miaka mingi kutokana na kaka yao Ayubu Mwenda kwenda tofauti na wanafamilia wengine.

Akizungumza kwenye shamba la familia marehemu mzee Mwenda Kasesela alisema kuwa kaka yao Ayubu Mwenda na wanafamilia wote kwa pamoja wamekaa na kufikia makubariano ya kugawana sawa ardhi ambayo ipo katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli.

“Kwa leo nimefalijika kuona familia hii imeamua kumaliza mgogoro huu ambao ulikuwa hauna afya katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi hawa kwa kuwa walikuwa wanapoteza muda mwingi kupigania mgogoro huu” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa familia hiyo inagombea hekali mia moja na hasini na tisa (159) ambazo waliachiwa na marehemu mzee wao mzee Mwenda na kusema kuwa Ayubu ambaye ndiye kaka yao mkubwa amekuwa kisababishi cha mgogoro huo.

Aidha Kasesela alimtaka afisa mtendaji na afisa tarafa kuhakikisha shamba hilo linagawawiwa kwa wake wote sita wa mzee Mwenda ili kuondo na kumaliza mgogoro huo kwa kugawa kwa usawa na haki ili kila mmoja apate haki yake.

“Mzee Mwenda alikuwa na wake sita hivyo shamba hilo litagawiwa kwa kufuata familia za akina mama wote kwa haki ili kumaliza hili tatizo na hakuna mtu mwingine ataleta mgogoro kwa kuwa nitalipeleka shauri hili mahakamani kuweka zuio la kuanzisha kesi yeyoyte ile katika shamba hilo” alisema Kasesela

Kwa upande wake msimamizi wa mirathi hiyo Sadiki Abdalah Mwenda alimshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kuasidia kutatua mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi bila kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

Naye askari mstaafu Hawa Mwenda ambaye ni mwanafamilia alimshukuru mkuu wa wilaya na kumuomba awafikishie salaam kwa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuongoza vizuri na kufanikisha wananchi wanyonge wafikiwe kirahisi na kutatuliwa matatizo yao.



No comments: