Kongamano la Wafanyabiashara, wachambuzi wa mambo, wachumi, wataalamu wa sheria, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kitaifa, washirika wa maendeleo na Taasisi za habari kutoka Tanzania na Uganda tarehe 6 - 7 Septemba 2019. Linakuhusu
Wakati huu Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano la wafanyabiashara kati ya Tanzania na Uganda litakalofanyika Septemba 6 hadi 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mkutano wa Biashara wa Tanzania na Uganda unawaweka pamoja Wafanyabiashara kutoka Uganda na Tanzania, wachambuzi wa mambo, wachumi, wataalamu wa sheria, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kitaifa, washirika wa maendeleo na Taasisi za habari.
Lengo kuu ya mkutano huu wa pamoja wa biashara ni kuunda jukwaa linalowezesha na kuruhusu sekta binafsi kutoka katika Tanzania na Uganda kushirikishana uzoefu, kuunda mitandao ya biashara, kubaini fursa na changamoto za biashara inayoendelea na uwekezaji, na kuonyesha bidhaa na huduma zao kwenye maonyesho.
Mfanyabiashra, Hapa utaunganishwa na masoko ya Mazao ya Chakula, Dawa za Binadamu, Mazao ya Maziwa, Ngozi, Dawa za Kuua Wadudu, Mafuta ya Kula yatokanayo na mbegu, Tumbaku, Mazao ya Ziwani na Baharini, n.k, yanayouzika katika masoko Kubwa la nchi za Uganda, Sudani Kusini na DRC.
Tanzania kama mzalishaji mkubwa wa Mzao ya chakula na ya viwandani, Inaweza kuingiza mazao katika viwanda na masoko ya nchi za Uganda, Sudani Kusini na DR Congo.
Swali la kujiuliza Je, Hili soko kubwa ambalo tayari waganda wameliona kwamba wanaweza kuja hapa Tanzania wakawaweka maraisi wetu pamoja wakasaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara ndio hapo sasa tunakutana na waganda Songwe wakinunua mahindi na kuyapeleka kuyauza Huko DRC na Sudani Kusini.
Watanzani wajitokeze sasa kufanya wenyewe biashara hizi.
Kuna haja gani ya kuwaruhusu “watukati” kuyatafutia masoko mazao ya chakula ambavyo yanazalishwa kwa jasho la watanzania wakati Watanzania wenyewe wanaweza kupeleka wenyewe kwenye hilo soko?
Vilevile Kuna fursa nyingi kama utalii, kufundisha Kiswahili Uganda pamoja na Kuuza mazao ya chakula.
Kwa kuzingatia hilo Serikali za Tanzania na Uganda zimeandaa kongamano hilo litakalosimamiwa na TPSF ambapo kutakuwa na maonyesho ya biashara na kuwakutanisha wafanyabiashara.
Kongamano hilo litakuwa ni fursa adhimu kwa nchi zote mbili na kutafuta suluhisho za vikwazo vya biashara kati ya nchi hizo na kuanzisha majukwaa ya ushirikiano yatakayowezesha kupeana uzoefu miongoni mwa wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa TPSF, Godfrey Simbeye alisema Tanzania inazo fursa nyingi zinazotakiwa kufanyiwa kazi.
Serikali hizi zimejitahidi kuboresha mazingira ya biashara ikiwa ni pamoja na kutekeleza mapendekezo ya Blueprint na kupunguza wingi wa ushuru zilizokuwa kikwazo kwa wafanyabiashara.
KWA HIYO, sasa ni wakati wa watanzania kuchangamkia fursa hizo zilizopo.
“Kuna fursa nyingi katika uwekezaji wa nchi na nchi ambao kama utatumika utazinufaisha nchi hizi mbili,”
#UGTZBusinessForum2019
No comments:
Post a Comment