ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 2, 2019

WAZIRI LUGOLA AAGIZA BODABODA ZOTE ZISAJILIWE NCHINI, AWATAKA TRAFIKI KUACHA VISINGIZIO UGUMU UKUSANYAJI FAINI BARABARANI ZINAPOFANYA MAKOSA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza Katibu wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bodaboda Mkoa wa Kilimanjaro (CWBK), Rashid Omary, alipokuwa anatoa pongezi kwa Waziri huyo, kuwasaidia kupata eneo la maegesho ya Bajaj na Bodaboda Shairifu, Mjini Moshi, leo. Mwezi uliopita, Lugola alitatua mgogoro uliopo kati ya Manispaa ya Moshi na CWBK kuhusiana na maeneo ya maegesho. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Khamis Issa, na wapili kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo, Zauda Mohammed. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (aliyevaa Kaunda suti), akikagua eneo la maegesho ya Bodaboda na Bajaj, Sharifu, Mjini Moshi, leo. Lugola aliambatana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Khamis Issa (kulia), kukagua maeneo ya Aghakan na Shairifu ambalo lilileta mgogoro kati ya Manispaa ya Moshi na Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bajaj Mkoani humo (CWBK), na kutatuliwa na Waziri huyo mwezi uliopita, mjini humo. Wapili kushoto ni Katibu wa CWBK, Rashid Omary. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimuaga Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bodaboda Mkoa wa Kilimanjaro (CWBK), Rashid Omary, mara baada ya kumaliza kukagua vituo vya Sharif una Aghakan vya maegesho ya Bodaboda na Bajaj, Mjini Moshi, leo.

No comments: