ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 5, 2019

Mahafali ya 41 ya NBAA yafana, Naibu Waziri Dkt. Kijaji atoa neno kwa wahitimu


Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akisoma hotuba wakati akifungua pamoja na kuwatunuku wahitimu kwenye mahafali ya 41 ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo  akizungumzia mafanikio pamoja na changamoto zinazowakabili kwa Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa mahafali ya 41 ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akitolea ufafanuzi kuhusu Bodi hiyo inavyofanya kazi zake wakati wa mahafali ya 41 ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji aliyokuwa akiitoa kwa wahitimu hiyo kwenye mahafali ya 41 ya Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji(kulia) akiwatunuku wahitimu wa  Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakati wa mahafali ya Bodi hiyo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo 
Wahitimu wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakisoma viapo vyao wakati wa mahafali ya 41 ya Bodi hiyo yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji  akiwapingeza baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya  Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakati wa mahafali ya 41 ya Bodi hiyo yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) akiwasili huku akiwa ameambatana na wenyeji wake wakiongozwa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo(kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno(wa pili kushoto) pamoja na Afisa Masoko na Mawasiliano kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Magreth Kageya(kushoto)

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa mradi wa kituo cha uhasibu kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam ulibuniwa kwa weledi mkubwa katika kuongeza wigo na fursa za mapato ya ndani sambamba na kuondoa matumizi yasiyo ya lazima ya kukodi majengo kwa ajili ya ofisi, kumbi na madarasa katika kuendesha shughuli zao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 41 ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam Dkt. Kijaji amesema kuwa utaalamu wa viongozi katika masuala ya fedha uliwasaidia na kutumika kama kichocheo kikubwa cha kubuni mradi huo ambao utawanufaisha watanzania wengi.

Aidha amewapongeza Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi ambao wamekuwa wabunifu katika utendaji kazi na kupambana na changamoto na kuhakikisha sekta hiyo nyeti inaendelea kufanya vizuri zaidi.

Kwa upande mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo amesema kuwa Serikali ya awamu tano chini ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli kupitia Wizara ya Fedha imeendelea kuwahudumia katika mambo mbalimbali ikiwemo uwezeshaji wa fedha na ushauri.

Amesema kuwa wahitimu wameendelea kuongezeka kutoka mwaka hadi mwaka na hiyo ni kutokana na mafunzo bora yanayotolewa na kituo hicho, na wameweza kutoa viongozi wahasibu katika sekta mbalimbali.

Awali akieleza mafanikio ya kituo hicho Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius Maneno amesema kuwa mazingira ya kusomea katika kituo hicho ni faafu na wataendelea kushirikiana na bodi ya wakurugenzi katika kusimamia maadili ya taaluma hiyo kwa kuzingatia sheria.

Vilevile amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi bora wa Bodi hiyo pamoja na kuzingatia maadili na mafunzo waliyopewa katika maeneo ya kazi wanakoenda kutumikia.

No comments: