Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akipata maelezo kutoka kwa kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi kwa namna gani watatengeneza barabara hiyo ili ichochee maendeleo kwa wananchi
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimuonyesha kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi kwa namna gani daraja hilo lipo hatarini kubomoka
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikagua moja ya madaraja ambavyo yamelalamikiwa kwa ubovu
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
JUMLA ya milioni mia tisa
ishirini na moja zinatumika katika kutatua Tatizo la barabara kuanzia Mkuta
hadi Mpangatazara kwa kiwango cha changalawe katika jimbo la Mufindi Kaskazini
kwa lengo la kurahisisha shughuli za kimaendeleo ambazo zimekuwa zikihusisha
barabara hiyo.
Akizungumza kwenye mikutano
ya hadhara ya mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa,kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi
Selemani
Mjohi alisema kuwa pesa tayari imepatika
na tayari wameshawapata wakandarasi ambao watatengeneza barabara hizo.
“Mheshimiwa mbunge
na wananchi wako mwezi huu wa kumi tunaanza kutengeneza barabara hii ambayo
imekuwa kimbilio la maendeleo kwa wananchi wa jimbo hili hasa katika biashara
ya usafirishaji wa zao la mbao ambalo ni chanzo kikubwa cha mapato kwa wananchi
wa jimbo la Mufindi Kaskazini” alisema Mjohi
Mhandisi Mjohi
alisema kuwa barabara hiyo inayotengenezwa itapita katika vijiji vya Ifwaji,Ifupira,Kidete,Ikanga,Ihanu,Ibwanzi,Lulanda,Isipii
na Mpanga Tazara kwasababu vijiji hivi vipo barabarani kabisa lakini vijiji
zaidi ya arobain vitanufaika na barabara hiyo kimaendeleo.
“Barabara hii
ikikamilika itahudumia zaidi ya vijiji arobaini ambavyo vipo pembezoni au
vinazungukwa kwa namna moja au nyingine na barabara hii ambayo imegharimu
mamilioni ya pesa ambazo zimetafutwa na mbunge wa jimbo hili” alisema Mjohi
Kwa upande
wake mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa aliwahakikishia
wananchi kuwa barabara hiyo itatengenezwa kwa kuwa fedha ametafuta na
amewakabidhi kwa TARURA wilaya ya Mufindi na tayari wameshapata wakandarasi
wawili ambao watatengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha changalawe.
“Mimi mbunge
wanu nimeshafanya kazi yangu ya kutafuta fedha nimepata na nimekabidhi kwa
wataalam hivyo kazi iliyobakia ni kuhakikisha wataalum wanasimamia vilivyo
barabara hii ili ijengwe kulinga na gharama ambazo zimetolewa” alisema Mgimwa
Mgimwa mgimwa alisema kuwa barabara hiyo
inaumhimu mkubwa kwenye biashara ya zao la mbao kwa kuwa ndio baishara kuu
inayofanyika katika barabara hiyo na kuwakumbusha wananchi kuwa barabara hiyo
ni yao na wanapaswa kuisimamia.
Nao wananchi
waliendelea kumkubusha mbunge umuhimu wa barabara hiyo kimaendeleo kwa kuwa
wananchi wamekuwa wakiitumia katika shughuli za kimaendeleo za kila siku.
No comments:
Post a Comment