Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango waendelea jijini Arusha katika ngazi ya Makatibu Wakuu. Mkutano katika ngazi hiyo ulikuwa wa siku mbili na umemalizika leo.
Pamoja na mambo mengine, mkutano umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 11 na 12 Oktoba 2019.
Pichani; wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka Rwanda, Balozi Richard Masozera akiongoza mkutano huo, wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Miundombinu, Mhandisi Steven D. M. Mlote, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia sekta za uzalishaji na jamii, Mhe. Christophe Bazivamo na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara inayoshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Kenya, Bw. Rafael Kanoth.
Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akisaini taarifa ya mapendekezo mbalimbali katika mkutano huo kwaajili ya kuwasilisha taarifa hiyo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri. Pembeni yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akishuhudia zoezi la utiaji saini.
Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen P. Mbundi pamoja na wajumbe wengine wa mkutano wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa (kushoto) pamoja na sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wakifuatilia majadiliano.
Sehemu nyingine ya wajumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano katika mkutano.
Viongozi wa ujumbe wa mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wakikamilisha zoezi la utiaji saini wa taarifa ya mapendekezo ya mkutano huo.
No comments:
Post a Comment