Kama wewe unachagua mwanaume mwenye kazi, nyumba nzuri, gari na mshahara, elewa kuwa hata wanaume nao wanahitaji na wanachagua mwanamke mwenye kujitambua, mwanamke mwenye kujisimamia. Wanataka mwanamke mwenye kazi, mwanamke ambaye anaweza akasimama yeye mwenyewe hata kama mwanaume atakuwa kwenye matatizo ya kiuchumi au kiafya.
Kwa sasa hakuna mwanaume ambaye anapenda kuoa au kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye yupoyupo, hana kazi. Japo kuna wanaume wengine wanaopenda wanawake wao wasifanye kazi, lakini kwa ujumla wake na hali ya sasa, wengi wana-tamani yule ambaye atape-nda kujishu-ghu-lisha.
Kama wewe ni binti na huja-olewa au hujata-mkiwa habari za kuolewa, basi jiulize sana inawe-zekana mwenendo na tabia yako ya kuchagua wachumba na kutaka mambo makubwa ndiyo hasa inakufelisha. Mwingine unaweza kukuta ukichagua mwanaume wa kukuoa kwa mbwembwe nyingi kwa sababu unajiona bado binti, bado unalipa lakini kama hujui ndugu yangu muda unaenda na mambo yanazidi kubadilika kila kukicha.
Simaanishi usiwe na chaguo sahihi la hasha, ila jaribu kuangalia maisha nje ya muonekano wa mtu kwa sababu unaweza kuchagua mwanaume mwenye kazi, nyumba na gari zuri lakini mwisho wa siku akawa hana mapenzi ya kweli. Nini kitakachofuatia kama siyo penzi lako kuwa la mateso? Kwa binti ambaye anahitaji kuolewa si vyema sana akaangalia pesa, mali au elimu ya unayetaka akuoe bali angalia utu na namna ambavyo mwanaume anakujali.
Ana upendo? Ana uwezo mzuri wa kufikiri katika maisha ya baadaye? Unaposhiriki kwenye mafanikio ya mumeo inakuwa ni jambo zuri na la kujivunia kuliko kukuta kila kitu kikiwa kwa mwanaume, hii itakufanya uwe kama unanyanyasika.
ata ikitokea mmekwaruzana kidogo basi anakutimua na matusi juu kuwa huna chako pale. Na ukiangalia katika uhalisia huna chako zaidi ya wewe na mabegi yako ya nguo. Usijione kama ni mwanamke mwenye bahati, furaha na raha sana kwa kumpata mwanaume ambaye umemkuta na kila kitu, sikia uchungu na mwambie au mfanye jambo fulani ambalo na wewe utashiriki kwa asilimia zote. Kidogo itakusaidia.Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri!
Instagram na Facebook; Erick Evarist, Twitter: ENangale. SIMAANISHI usiwe na chaguo sahihi la hasha, ila jaribu kuangalia maisha nje ya muonekano wa mtu kwa sababu unaweza kuchagua mwanaume mwenye…GPL
No comments:
Post a Comment