Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu Mkoani Mwanza. Kulia ni Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Balozi Mstaafu
Mhe. John Haule, Mhe. Khadija Mbarak na Mhe. Alhaj Yahya Mbila.
Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu Mkoani Mwanza.
Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Balozi Mstaafu Mhe.John Haule, akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma, wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Dkt. Philemon Sengati wakati wa kikao kazi kati yake na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu kabla ya kikao kazi kati yake na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magu.
Na Happiness Shayo, Magu
Watumishi wa Umma nchini wametakiwa kutumia vizuri rasilimali zilizopo katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya kiutumishi iliyopo.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Magu mkoani Mwanza.
“Tujenge uzalendo kwa kutumia vizuri rasilimali wezeshi katika utendaji kazi wetu, tupende na kuthamini ili kuharakisha maendeleo ya taifa” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi hao kuwa wavumilivu katika utendaji kazi kwani Serikali inatambua changamoto zinazowakabili na inaendelea kuzifanyia kazi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Dkt. Philemon Sengati amemuahidi Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa kwa maslahi ya Taifa.
“Nimefarijika mno na hii ziara na nimeyapokea maelekezo kwa moyo mkunjufu kabisa, na nikuhakikishie kwamba tutaendelea kufanya kazi kwa ubunifu” Dkt. Sengati amefafanua.
Ziara ya kikazi ya Mhe. Mwanjelwa mkoani Mwanza ni utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake ya kuhimizi uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
No comments:
Post a Comment