Wachezaji wa timu ya Kidamali inayoshiriki ligi ya mkoa wa Iringa maarufu kama ASAS SUPER LEAGUE ambapo mchezaji wa timu hii Emanuel Geka anaongoza kwa ufungaji wa magoli hukupia timu ya kidamali ikiwa imefuzu hatua ya nane bora ya ASAS SUPER LEAGUE
Wachezaji wa timu ya Kidamali inayoshiriki ligi ya mkoa wa Iringa maarufu kama ASAS SUPER LEAGUE ambapo mchezaji wa timu hii Riziki Kelvin anaongoza kwa ufungaji wa magoli huku pia timu ya Isiman ikiwa imefuzu hatua ya nane bora ya ASAS SUPER LEAGUE
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
WACHEZAJI nane kutoka timu za Mafinga Academy,Kidamali
fc,Kalinga Fc,Isimani Fc, Mapanda Fc na Irole fc wanafukuzia tuzo ya mfungaji
bora wa mashindano ya kugombea kombe la bingwa wa mkoa yanajulikana kwa
jina la Asas Super League 2019 (ASL 2019).
Wachezaji hao vinara Emanuel Geka wa Kidamali anamagoli 8, Luka
Duma (Irole fc) na Riziki Kelvin wa Isimani Fc wana magoli 7 kila mmoja Baraka Athumani
kutoka Mafinga Academy na Vicent Madembo (Mapanda Fc) kila mmoja wana goli 5,
Kelvin Msafiri (Kalinga Fc),Conrodgers (Irole Fc)na Mohamed Rashid (Isimani fc)
wameonyesha uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu ambapo hadi sasa kila mmoja
amefanikiwa kufunga magoli 4 katika michezo waliyocheza.
Licha ya ushindani mkali katika mashindano hayo katika
ufungaji mchezaji wa Kidamali fc Emanuel Geka anakimbizwa kwa karibu na mchezaji
Riziki Kelvin wa Ismani ambaye anamagoli saba na alikuwa mfungaji bora msimu
uliopita.
Mchezaji wa Kidamali fc Emanuel Geka amefunga magoli mengi akiwa
katika uwanja wa kidamali tofauti na akiwa anacheza nje ya uwanja wao wa
nyumbani hivyo amekuwa mmoja ya wachezaji ambao wanautumia vizuri uwanja wa
nyumbani kufumania nyavu za wapinzani.
Katika mashindano hayo hadi sasa timu ya soka ya Irole Fc ndio
kinara wa magoli mengi kwa kuwa na magoli 18 katika michezo 7 iliyocheza
ikifatiwa na timu ya soka ya Isiman Fc yenye mabao 17 huku Kidamali Fc wakiwa
na mabao 13 na hizi timuzote zinatoka katika kundi B na zimefuzu hatua ya nane
bora ya Asas Super League.
Timu za Acosato ndio timu iliyoruhusu magoli mengi kwenye
michezo yao kwa kufungwa goli 15 huku ikifuatiwa na timu ya African wonders
ambao wamefungwa magoli 14 huku zikifuatiwa na Magulilwa na mapanda fc ambazo
zote zimefungwa magoli 12 kila.
Aidha ligi hiyo hadi kufikia sasa jumla ya magoli 170 yamefungwa
na timu zote zinazoshiriki ligi ya Asas Super League msimu wa 2019/2020
Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya maziwa ya Asas bingwa
atapata kombe na sh. 2,000,000,jezi seti moja,mipira mitatu na cheti, na nafasi
ya kushiriki ligi ya mabingwa wa mikoa.
Mshindi wa Pili shilingi 1,000,000, Mipira 2, Jezi Seti 1, Cheti
cha Ushiriki huku Mshindi wa Tatu - Tsh 500,000/=, Jezi Seti 1, Cheti cha
Ushiriki na zawadi nyingine ni kwa wanahabari wameyatangaza vyema
mashindano hayo kama ifuatavyo Mwandishi bora blog, Mwandishi bora wa luninga ,
Mwandishi bora Redio kipindi cha michezo na Mwandishi bora gazeti watapata sh.
50,000 kila mmoja.
Lakini pia kutakuwa na zawadi kwa kipa bora, mchezaji bora
wa mashindano, mwamuzi bora,mfungaji bora , timu yenye nidhamu itaondoka na
zawadi pia.
No comments:
Post a Comment