Mrema ametoa kauli hiyo jana Jumapili wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bi Anna Mgwhira, katika kijiji cha Kiraracha, jimbo la Vunjo mkoani humo, ambapo ameonya kuwa endapo hali hiyo itaendelea, basi huenda kukatokea machafuko huko mbeleni.
Mrema ameyasema hayo leo akizungumza kuhusu uchaguzi huo kwamba hatendewi haki licha ya kuwa na kijiji kimoja pekee.
Mrema ambaye chama chake kimeshiriki katika uchaguzi kwenye kijiji cha Kiraracha pekee ambako ndiko anakoishi, akichuana na CCM, amedai kuwa aliamua kushiriki uchaguzi huo ili kumsaidia Rais John Magufuli lakini hajatendewa haki.
“Hali ni mbaya, kwani mimi nilikuja kushiriki uchaguzi huu kwa nia njema kumsaidia rais wangu kwa sababu walitaka kuonyesha kuwa hakuna utawala bora, watu walisusa na kugoma, mimi nikasema ingawa sina halmashauri nibaki na kijiji hiki kimoja.
Aliongeza, “Nilisema ushindani uwe kwenye sanduku la kura, lakini haikutokea hivyo, magari yote ya serikali ya Moshi yamehamia Kiraracha, kuna mawakala wangu wametolewa kwenye vituo, hali ikiwa hivi nchi itaharibika.
Akizungumzia malalamiko hayo, msimamizu wa uchaguzi Moshi Vijijini, Juma Tukosa, amesema hali inakwenda vizuri na wakala anayemlalamikia Mrema, alikuwa anakunywa pombe katika eneo la kituo na kuambiwa aziondoe, ndipo alipoanza kulalamika anaondolewa kituoni.
“Hakuna wakala aliyeondolewa, ila katika kituo kimoja wakala wa TLP, alikuwa na bia tatu ndani ya kituo, alipoambiwa aziondie bia hizo, akaanza kulalamika anaondolewa lakini hajaondolewa bado yupo kituoni,” amesema Tukosa. GPL
No comments:
Post a Comment