Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kutunukiwa Shahada ya heshima ya Udaktari wa Falsafa (Phd) katika wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) tarehe 21/11/2019 jijini Dodoma. Rais Magufuli ametunukiwa PhD hiyo ikiwa ni kutambua mchango wake katika maendeleo ya nchi ambapo anakuwa mtu wa tatu kutunukiwa Shahada ya heshima ya Uzamivu na chuo hicho akitanguliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete na Mzee Rashid Mfaume Kawawa.
VYUO vikuu nchini vimetakiwa kufanya tafiti mbalimbali kulingana na mahitaji na vipaumbele vya nchi na kupunguza kutegemea misaada ya nje kwenye tafiti zao kwakuwa wanaotoa misaada ndio wanaowapa ajenda ya utafiti.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Cheti cha Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PhD) katika Sayansia wakati wa Mahafali ya 10 ya chuo hicho tarehe 21/11/2019 jijini Dodoma. Rais Magufuli ametunukiwa PhD hiyo ikiwa ni kutambua mchango wake katika maendeleo ya nchi ambapo anakuwa mtu wa tatu kutunukiwa Shahada hiyo na UDOM akitanguliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete na Mzee Rashid Mfaume Kawawa.
Hayo yamesemwa Alhamisi Novemba 21, 2019 na Rais John Magufuli alipokuwa akizungumza katika mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Dododma (UDOM), baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa katika Sayansi ya chuo hicho.
Kutoka kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mke wa Rasi Msaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakifuatilia Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma ambapo Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika Sayansi tarehe 21/11/2019 jijini Dodoma.
“Ili kukuza uwezo wa kujitegemea katika gharama za utafiti anzisheni na imarisheni mifuko yenu ya fedha za utafiti, tafuteni njia mbalimbali za kuimarisha mifuko hiyo ikiwemo kutumia taaluma zenu mlizonazo, serikali kwa upande wake itaendelea kusaidia kwa kuongeza mchango wake katika mfuko wa utafiti wa kitaifa nchini ili kwa kushirikiana na jitihada za vyuo vikuu katika kuimarisha uwezo wetu wa ndani wa kugharamia tafiti zetu zinazobeba ajenda zetu wenyewe.
“Tafiti na matokeo ya tafiti hizo zitakuwa na maana tu ikiwa zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wetu, anagalieni namna tafiti zenu zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya taifa, bainisheni matatizo na tafuteni majibu ya yanayowakabili wazalishaji mbalimbali kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji madini na wenye viwanda” amesema Raisi Magufuli.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (kulia) wakati wa hafla ya Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) tarehe 21/11/2019 jijini Dodoma. Katika mahafali ya hayo Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametunukiwa Shahada ya heshima ya Udaktari wa Falsafa (Phd) katika Sayansi ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuleta maendeleo ya nchi
No comments:
Post a Comment