ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 7, 2019

TANZANIA NA MALAWI WASAINI MAKUBALIANO YA KIBIASHARA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Malawi Mhe. Ralph Jooma, wakati alipokutana nae pamoja na ujumbe wake katika ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Malawi, Mhe. Ralph Jooma, akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe, pamoja na timu ya wataalamu kutoka Sekta ya Uchukuzi hapa nchini wakati alipokutana nao katika ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leonard Chamriho, akitoa taarifa ya utekelezaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Malawi, Mhe. Ralph Jooma, hususan ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika Barabara, Bandari ya Dar es Salaam na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), wakati walipokutana katika ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Malawi Mhe. Ralph Jooma, wakibadilishana makubaliano ya ushirikiano waliosaini kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya kuimarisha biashara na mahusiano ya kijamii kwa kutumia miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam, Barabara pamoja na Safari za Ndege za ATC, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe, akimkabidhi zawadi Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Malawi Mhe. Ralph Jooma, mara baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya kuimarisha biashara na mahusiano ya kijamii kwa kutumia miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam, Barabara na Safari za Ndege za ATC jijini Dar es Salaam.

No comments: