Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisoma hotuba yake wakati kikundi hicho kilipokabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha waototo wenye mahitaji mwalimu cha Buhangija wilayani Shinyanga Novemba 10, 2019. Kushoto ni Mgeni rasmi katika makabidhino hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Umoja wa wake wa viongozi nchini Tanzania ‘Ladies of New Millenium Women Group’ umekabidhi madarasa manne yenye thamani ya shilingi milioni 65.8 na matundu 10 ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 21 yanayoendelea kujengwa katika mabweni ya shule ya Msingi Buhangija Jumuishi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga ambayo ni maalumu kwa watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye ualbino,viziwi na wasioona.
Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (wakwanza kulia), akiwaongoza wake za viongozi akiwemo Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako (wapili kulia)wakigawa chakula kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Buhangija Jumuishi, Mkoani Shinyanga.
Wake wa viongozi wakiongozwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (wakwanza kulia), wakigawa chakula kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Buhangija Jumuishi, Mkoani Shinyanga.
No comments:
Post a Comment