Advertisements

Thursday, December 5, 2019

WAFANYABIASHARA, WAWEKEZAJI MKOANI MOROGORO WAWASILISHA CHANGAMOTO ZAO KWA MAWAZIRI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (wa kwanza kulia) wakiwa pamoja na Manaibu Waziri wakipata maelezo kutoka kwa Sajenti Esther Mbugura kuhusiana na vifaa vinavyotumika kwa ajili ya kuzimia moto wakati wa Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji Morogoro.
Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali wakiwasili ukumbini kwa ajili ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji kwa lengo la kusikiliza changamoto zao uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Glonency Mkoani Morogoro tarehe 12 Disemba, 2019. Kushoto ni Mkuu wa mkoa huo Mhe. Loata Ole Sanare.
Baadhi ya Watendaji wakuu wa Serikali wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuingia ukumbini kwa ajili ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji kwa lengo la kusikiliza changamoto zao uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro.
Baadhi ya Manaibu Waziri na Mawaziri wa Wizara walioshiriki katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji wakiwasikiliza wachangiaji mbalimbali walioalikwa katika mkutanouliolenga kusikiliza changamoto za Wafanyabiashra uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro tarehe 12 Disemba, 2019.
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia majadiliano ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza na kutatua changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro 
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wakifuatilia majadiliano ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza na kutatua changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro
Afisa Masoko wa Royal Agri Company, Elizabeth Priscus akichangia hoja ya kuwawezesha Wahitimu kujihusisha katika shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali mkoani Morogoro katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency.
Waziri wa Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki wakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole Sanare wakiwa katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro
Mmoja wa Wafanyabiashara, Mwadhini Myanza akichangia hoja ya uwepo wa viwanda vya pamba katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro
Mjumbe wa TCCIA, Anthony Fuime akichangia hoja kuhusu umuhimu wa kuwa na mipango inayotekelezeka katika ngazi ya Halmashauri wakati wa Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments: