Advertisements

Thursday, December 5, 2019

WAKIMBIZI WAANZA KUHAKIKIWA DAR ES SALAAM


Afisa Mkuu wa Uendeshaji na Utawala wa Makambi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Stephen Msangi, akifafanua jambo kabla ya kuanza zoezi la uhuishaji takwimu za wakimbizi waishio Dar es Salaam jana, katika Ofisi za Shirika la Relief of Development Society (REDOSO), eneo la Biafra, Kinondoni.
Baadhi ya wakimbizi waishio Dar es Salaam wakisubiri kuhuisha takwimu zao kwenye Ofisi za Shirika la Relief of Development Society (REDOSO), eneo la Biafra, Kinondoni.
Baadhi ya wakimbizi waishio Dar es Salaam wakisubiri kuhuisha takwimu zao kwenye Ofisi za Shirika la Relief of Development Society (REDOSO), eneo la Biafra, Kinondoni.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji na Utawala wa Makambi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Stephen Msangi, akizungumza jambo kabla ya kuanza zoezi la uhuishaji takwimu za wakimbizi jijini Dar es Salaam katika Ofisi za Shirika la Relief of Development Society (REDOSO), eneo la Biafra, Kinondoni. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uendeshaji Makambi na Makazi, Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Nsato Marijani na Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni na Usalama, Kanali Rajabu Maisha.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uendeshaji Makambi na Makazi, Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Nsato Marijani (katikati), akisalimiana na Afisa Mkuu wa Uendeshaji na Utawala wa Makambi, Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Stephen Msangi, baada ya kufika katika Ofisi za Shirika la Relief of Development Society (REDOSO), eneo la Biafra, Kinondoni ili kusimamia uhuishaji taarifa za wakimbizi waishio Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni na Usalama, Kanali Rajabu Maisha. (PICHA NA VERONICA MWAFISI-MOHA)

No comments: