ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 26, 2020

TANZANIA COMMUNICATIONS REGULATORY AUTHORITY

TAHADHARI KWA UMMA 

NDUGU WATANZANIA;

KAMA MNAVYOFAHAMU, LAINI ZA SIMU AMBAZO HAZIJASAJILIWA KWA KUTUMIA NAMBA YA KITAMBUSHO CHA TAIFA (NIDA) NA KUTHIBITISHWA KWA ALAMA ZA VIDOLE ZILIANZA KUZIMWA TAREHE 20 JANUARI, 2020 USIKU NA ZOEZI LINAENDELEA.

HAKIKI TENA USAJILI WA LAINI ZAKO KWA KUPIGA NAMBA *106# NA UCHUKUE HATUA STAHIKI SASA.

1.0 KWA WALIOSITISHIWA HUDUMA ZA LAINI ZAO ZA SIMU KUANZIA TAREHE 20.01.2020 WANAWEZA PIA KUENDELEA NA UTARATIBU WA USAJILI KWA LENGO LA AMA KURUDISHA LAINI ZAO ZILIZOFUNGWA KAMA ZITAKUWA BADO ZIPO AU KUPATA LAINI MPYA. ZOEZI HILI NI ENDELEVU.

2.0 KWA WATUMIAJI/WAOMBAJI (WATANZANIA) WAPYA WA LAINI ZA SIMU WATAENDELEA KUSAJILIWA MUDA WOTE KWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA TAIFA NA KUHAKIKIWA KWA ALAMA ZA VIDOLE. HUDUMA HIYO NI ENDELEVU PIA.

3.0 MATUMIZI SAHIHI YA VITAMBULISHO WAKATI WA USAJILI WA LAINI ZA SIMU (ZINAZOTUMIKA AMA KWA AJILI YA MAWASILIANO YA SIMU ZA SAUTI AU VIFAA VYA MAWASILIANO MENGINE) UKO KATIKA MAKUNDI YAFUATAYO:-


3.1 Sisi wa-Tanzania kitambulisho chetu ni kile cha Taifa
kitolewacho na NIDA kwa vigezo vyao;

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

ISO 9001:2015

CERTIFIED

3.2 Kwa wageni wanaokaa hapa nchini chini ya miezi sita wanasajili laini za simu kwa kutumia namba za Hati zao za kusafiria na kuhakiki kwa alama za vidole;

3.3 Kwa wageni wanaokaa zaidi miezi sita wanatumia vitambulisho (Legal Resident ID) ambavyo hupewa na NIDA (Hii ni kwa mujibu wa utaratibu wa Uhamiaji na NIDA);

3.4 Kwa wanadiplomasia wanatumia Hati zao za kusafiria pamoja na vitambulisho vyao vinavyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje; na

3.5 Kwa wakimbizi wanatumia vitambulisho vyao ambavyo hupewa na NIDA (Hii ni kwa mujibu wa utaratibu wa Uhamiaji na NIDA),

4.0 KATIKA KUJIRIDHISHA KUWA WALIOSAJILI LAINI ZAO ZA SIMU WAMETUMIA VITAMBULISHO SAHIHI, TCRA KWA KUSHIRIKIANA NA WATOA HUDUMA ITAFANYA ZOEZI LA KUHAKIKI LAINI ZOTE ZITAKAZOKUWA ZIMESAJILIWA ILI KUWAONDOA WALE WALIOSAJILI LAINI ZAO AMA KWA KUTUMIA VITAMBULISHO VYA WATU WENGINE AU KWA KUTUMIA KITAMBULISHO TOFAUTI SAMBAMBA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA.

5.0 IKUMBUKWE PIA KWAMBA KUSAJILI LAINI YA SIMU KWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA MTU MWINGINE NI KOSA SANJARI NA KUPEWA LAINI ILIYOSAJILIWA NA MTU MWINGINE.

6.0 ONYO NA TAHADHARI ZINAENDELEA KUTOLEWA KWA MAKUNDI YOTE YALIYOORODHESHWA KWENYE KIPENGELE CHA 3.0 HAPO JUU, KUTOTUMIA KITAMBULISHO KISICHOKUHUSU WAKATI UNASAJILI LAINI ZAKO ZA SIMU (ZINAZOTUMIKA AMA KWA AJILI YA MAWASILIANO YA SIMU ZA SAUTI AU VIFAA VYA MAWASILIANO MENGINE).

Imetolewa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) 24 Januari, 2020

No comments: