Advertisements

Wednesday, January 22, 2020

Wamiliki Mabasi Wanaotuhumiwa Kuhujumu Reli Wajisalimisha Polisi

MKUU wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, amesema tayari wamiliki wa mabasi wanaotuhumiwa kuhujumu miundombinu ya reli wameripoti kituo cha polisi Bomang’ombe wilayani Hai.

Wamiliki hao ni Clemence Mbowe anayemiliki mabasi ya Machame Safari na Rodrick Uronu anayemiliki mabasi ya Limu Safari.

Amesema: “Mpaka sasa hivi (jana) tunavyozungumza wanasikilizwa na jeshi la polisi, na jeshi la polisi nao wanaendelea kufanya kazi yao ya mahojiano kujua ukweli wa jambo hili na kulifikisha mwisho kwa hiyo, hiyo ni hatua ya kwanza na hatua nyingine baada ya mahojiano zitafuata.
“Sasa wao ndiyo watafika mbele ya vyombo vya dola waseme ni kweli ama si kweli, na sisi tutawaambia kwa nini hizo taarifa tumezipata na tumezipataje. Jambo kubwa ni kwamba haya yanafanyika ili kuilinda miundombinu hii inayojengwa kwa gharama kubwa.”

Ole Sabaya amesema hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya watu watakaoendelea kuhujumu miundombinu ya taifa.

Jumapili ya Januar 19, 2020, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, aliagiza wamiliki wawili wa mabasi kukamatwa kwa tuhuma za kuunda genge la uhalifu kwa lengo la kuhujumu miundombinu ya reli ili kuathiri usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar es Salaam – Moshi hadi Arusha.

GPL

No comments: