Advertisements

Tuesday, January 21, 2020

MBWANA ALLY SAMATTA RASMI ASTON VILLA


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, baada ya kusubiri kwa muda, hatimaye ametia saini ya kuichezea Aston Villa kwa mkataba wa miaka minne.

Usiku wa kuamkia leo, Januari 21, 2020, klabu ya Aston Villa kupitia ukurasa wake wa Twitter na Instagram, wamemtambulisha Samatta.

Nahodha huyo wa Taifa Stars anajiunga na Villa akiwa na kibarua kizito cha kuhakikisha timu hiyo inajiondoa katika janga la kushuka daraja

Samatta anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu England akitokea Genk ya Ubelgiji.
Tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ilipotangazwa kuwa ‘Samagoa’l atajiunga na Villa, Watanzania kutoka kona mbalimbali za dunia walikuwa wakisubiri kwa hamu kutimia kwa usajili huo.

Villa kwa sasa ipo nafasi ya 18 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England na wamemchukua Samatta kwa lengo la kumaliza tatizo lao katika safu ya ushambuliaji msimu huu.GPL

No comments: