Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa akifungua mafunzo ya siku moja kuhusu kuzuia na kupambana na rushwa kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU).
Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma kutoka TAKUKURU Bw. Joseph Mwaisalo ndiye aliyekuwa mwezeshaji wa mafunzo hayo akiwa amefuatana na Bi. Stella Mpanju. Bw. Mwaisalo amesisitiza kwamba rushwa ni zaidi ya hongo na kuwataka watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kujiepusha na vitendo vya rushwa kutoka na unyeti wa Ofisi hiy
Washiriki wa Mafunzo hayo walikuwa ni Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Wakuu wa Vitengo, Mawakili wa Serikali na Watumishi wa Kada mbalimbali.
baadhi ya Watumishi kutoka kada mbalimbali wakishiriki mafunzo kuhusu kuzuia na kupambana na rushwa. Mafunzo hayo yamefayika Dodoma.




No comments:
Post a Comment