
Marin, akiwa kiongozi mkuu wa serikali mdogo kuliko wote duniani kwa kuongoza nchi hiyo akiwa na umri wa miaka 34, amependekeza pia kwamba muda wa kazi uwe saa sita badala ya nane kwa siku.
Kiongozi huyo mwenye mtoto mmoja anaongoza muungano wa vyama vya mlengo wa kati-na-kushoto akiwa na viongozi wengine wa vyama vinne ambavyo vitatu vinaongozwa na wadada wenye umri wa chini ya miaka 35.
Katika mahojiano alisema: “Naamini wananchi wana haki ya kutumia muda wao mwingi na familia zao, wapenzi wao na mambo mengine katika Maisha kama vile hobby na utamaduni. Hii itakuwa hatua kubwa kwetu katika Maisha ya kazi”.
Kabla ya kuwa Waziri Mkuu Marin alikuwa Waziri wa Uchukuzi wa Finland, ambapo hata huko wizarani alipigania suala la kuwa na siku chache za kufanya kazi katika wiki ili kuongeza ufanisi na tija.
Hivi sasa nchini Finland kufanya kazi saa nane kwa siku na siku tano kwa wiki ni jambo la kawaida. Pendekezo hilo limeungwa mkono mara moja na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Bi. Li Andersson, ambaye ni kiongozi wa chama cha Left Alliance.
No comments:
Post a Comment