Advertisements

Tuesday, February 18, 2020

RPC KILIMANJARO NA RIO KILIMANJARO WAKIANGALIA GARI LILILOTUMIWA NA HAYATI JULIUS KAMBARAGE NYERERE KUTAFUTA UHURU WA TANGANYIKA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Salum Hamduni, akimuonyesha Mkuu wa Uhamiaji, Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi Tunu Ng’ondya mandhari ya ndani ya gari lililotumiwa na Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kutafuta Uhuru wa Tanganyika, gari hilo limepaki Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi, mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Salum Hamduni, akisoma taarifa fupi iliyobandikwa ndani ya gari lililotumiwa na Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kutafuta Uhuru wa Tanganyika,kulia ni Mkuu wa Uhamiaji, Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi Tunu Ng’ondya, gari hilo limepaki Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi, mkoani Kilimanjaro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments: