Advertisements

Sunday, February 16, 2020

ZIARA YA WAZIRI ZUNGU WILAYANI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiangalia mojawapo ya mabwawa ya majitaka yanayodaiwa na wananchi wa eneo la Buguruni Kisiwani kutokana na harufu mbaya na mazalia ya mbu na kusababisha magonjwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akikatiza juu ya daraja la kuvuka maji yanayotiririka kutoka viwandani eneo la Buguruni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akishuhudia uharibifu wa mazingira unaotokana na uchimbaji mchanga katika eneo la Tabata Segerea jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake wilayani Ilala ambapo ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kukaa na Mamlaka za Mabonde kukaa pamoja na kufanya tathmini ya namna ya kutatua changamoto ya uchimbaji mchanga kiholela jijini humo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza katika ziara yake eneo la Buguruni Kisiwani ambako kuna mabwawa ya majitaka yanayodaiwa na wananchi kuwa kero katika eneo hilo kwa kusababisha harufu mbaya na magonjwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akikagua eneo la mabwawa ya majitaka eneo la Buguruni Kisiwani yanayodaiwa kuwa kero kwa wananchi kwa kutoa harufu. (PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

No comments: