Advertisements

Thursday, May 28, 2020

FIFA yafafanua adhabu ya kutema mate

Zurich. Shrikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limetoa muongozo kwa vyama na mashirikisho ya soka duniani kuwa na uamuzi binafsi juu ya adhabu ya kutema mate katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya Corona.

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya FIFA, Pierluigi Collina katika barua yake kwa vyama na mashirikisho ya soka, amesema kuwa kamati hiyo haina mamlaka ya moja kwa moja juu ya adhabu kutokana na kosa hilo kufuatia mapendekezo yaliyotolewa hivi karibuni.

Kutokana na tatizo la virusi vya Corona, kundi kubwa la wadau wa soka limependekeza kuwa kosa la kutema mate liwe la kadi nyekundu iwe kwa mchezaji kumfanyia mwenzake au kutema popote pale uwanjani.

"Kutokana na uwezekano wa kusambaa kwa virusi vya Corona, waandaaji baadhi wa mashindano wameweka protokali ya kuwaepusha na kutema mate au vitendo vinavyohusiana na hivyo.
Kumtemea mtu mate ni kosa la kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa mujibu wa sheria 17 za soka. Hata hivyo utemaji mate unapokuwa haujaangukia katika namna hiyo, ni vigumu utekelezaji wa kutoa kadi ya njano kwa refa kwa sababu unaweza kutokea kokote ndani ya uwanja.

Kutokana na hilo mashindano yanapotoka kuweka protokali juu ya utemaji mate, uamuzi wowote wa kinidhamu unatakiwa kutolewa baada ya mechi na waandaaji wa mashindano, chama au shirikisho la soka la nchi husika," ilisema barua hiyo ya Collina.

Ligi mbalimbali zimeanza kurejea duniani baada ya kusimama tangu mwezi Machi, k ikiwa ni miongoni mwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kukabiliana na virusi vya Corna ambavyo vinasababisha ugonjwa wa Covid19 unaoweza kuwa chanzo cha homa kali ya mapafu. MWANASPOTI


No comments: