ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 24, 2020

MAABARA MPYA SASA KUPIMA SAMPULI 1800 ZA COVID-19 NDANI YA SAA 24-WAZIRI UMMY

"Upimaji wa Sampuli zote za Covid-19 umehamishiwa katika maabara Mpya ya Afya ya miiJamii (pichani juu) iliyopo Mabibo jijini Dares Salaam.
Mei 23, 2020 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua maabara hiyo. 
Maabara hii mpya ina uwezo wa kupima sampuli 1800 za Ugonjwa wa Covid -19 ndani ya masaa 24 tofauti na ile ya awali ilyokua na uwezo wa kupima sampuli 300 tu.
Waziri Ummy amesema katika maabara ile ya zamani moja ya Mashine za kupima sampuli za Covid-19 ilikua na hitilafu bila uongozi wa Maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati.
Aidha Waziri Ummy ameshuhudia zoezi la kuwapima na kuzungumza na madereva wa malori ambao wamefika kuchukuliwa sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa corona kabla ya safari nje ya Nchi na kuwahakikishia kupata majibu yao ndani ya saa 24.

No comments: