By Elizabeth Edward, MWANASPOTI
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imefichua kuanza uchunguzi juu ya matumizi mabaya ya fedha kiasi cha zaidi ya Shilingi 1 bilioni kilichotolewa na serikali na wadau wengine kwa ajili ya kufanikisha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya Umri wa miaka 17 (Afcon U17) zilizofanyika mwaka jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbung'o alisema kuwa fedha hizo ambazo kiasi kikubwa kilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, hakikutumika vizuri na wamegundua viashiria vya ubadhilifu.
"Lakini baada ya Mheshimiwa Rais kuonyesha mfano wa kuchangia, wako wadau wengine waliojitokeza.Kuna mashirika mbalimbali yalihusika kuchangia fedha.
Sasa zile fedha kweli zimetumika vibaya na taasisi inazo taarifa. Imechukua hatua za kufanya uchunguzi. Na huu uchunguzi uko vizuri. Tunawaita watu wote wanaohusika au wanaohisiwa kuhusika kwa namna yoyote ile ya ugawaji au usimamiaji wa hizo fedha.
Tunawaita wanakuja hapa, tunawahoji. Tunaendelea kukusanya nyaraka mbalimbali zinazoonyesha ukusaji wa ile fedha na matumizi yake zilivyotumika.Kwa hiyo niseme tu kwamba uchunguzi unaendelea na huu ni uchunguzi wa kijinai. Hawa watu wana hiari ya kuanza kurejesha hizo fedha lakini uchunguzi upo na unafanyika na wahusika wote wanaitwa Takukuru," alisema Brigedia Jenerali Mbung'o.
Rais Magufuli alitoa mchango huo wa fedha kulisaidia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuandaa fainali hizo zilizofanyika kuanzia Aprili 14 hadi 18 mwaka jana.
Cameroon waliibuka mabingwa wa mashindano hayo baada ya kuichapa Guinea kwa mikwaju ya penati 5-3 kufuatia timu hizo kutoka sare tasa katika dakika 120 za mchezo.

No comments:
Post a Comment