ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 12, 2020

BODI YA WAKURUGENZI YA IMF IMEIDHINISHA DOLA ZA KIMAREKANI 14.3 MSAMAHA WA KODI ZA MADENI KWA TANZANIA KUTOKANA NA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA CORONA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyakazi mbalimbali wa Serikali kabla ya kufungua Jengo la Ofisi za Makao Makuu ya TARURA mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua jingo la la Ofisi za Makao Makuu ya TARURA mjini Dodoma
PICHA NA IKULU

Na.Alex Sonna,Dodoma

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeidhinisha dola za Marekani milioni 14.3 za msamaha wa kodi za madeni.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akizindua Jengo la Wakala wa barabara Vijijini na Mijini (TARURA) lililopo katika mji wa kiserikali Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.

“Leo ninapozungumza tumepata fedha za msahama, Bodi ya Wakurugenzi ya IMF imeidhinisha leo dola za marekani milioni 14.3 za msamaha wa kodi wa madeni tuliyokuwa nayo na kwasababu tulipambana vizuri sana na ugonjwa wa corona” – amesema Rais Magufuli

Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa msamahaa huo umekuja wakati muafaka, na kuwa atamwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa IMF kwa niaba ya watanzania kwa lengo la kuwapongeza kwa kutambua juhudi za Tanzania.

Aidha amesema kuwa fedha hizo pia zitatumika katika kuendelea kupambana na janga la corona na kushugulikia katika maeneo mengine ambayo yatasaidia kumaliza tatizo la corona nchini.

No comments: