ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 9, 2020

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza afariki kwa mshtuko wa moyo akiwa na miaka 55

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameaga dunia, BBC

Kulingana na msemaji wa serikali, balozi Willy Nyamitwe, Rais Pierre Nkurunziza mwenye umri wa miaka 55 amefariki kwa mshtuko wa moyo kinyume na uvumi unaoenezwa.

Serikali ya Burundi imetangaza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza, katika ujumbe ulioandikwa katika mtandao wa Twitter, unaosema kwamba Agosti 8 "Timu ya madaktari walishindwa kunusuru maisha yake baada ya kupata mshutuko wa moyo."

Serikali ya Burundi imetangaza siku saba za maombolezo na ametuma salamu za ramirambi kwa familia.

Aidha, serikali inasema kuwa alilazwa hospitalini Jumamosi iliyopita.

Jumamosi, Bwana Nkurunziza, ambaye anapenda sana masuala ya michezo, alikuwa anahudhuria mashindano ya voliboli, katika uwanja ulio karibu na nyumbani eneo la Buye, mkoa wa Ngozi kaskazini mwa Burundi kabla ya kukimbizwa hospitali ya karusi katika mwa nchi hiyo jioni.

Bwana Mr Nkurunziza, baba ya watoto watano amega dunia huku mke wake Denise Nkurunziza akiwa anatibiwa kwa ugonjwa usiojulikana mjini Nairobi, nchini Kenya tangu Mei 28, afisa katika ofisi ya rais amezungumza na idhaa ya BBC ya Maziwa Makuu.

Bado haijafahamika ikiwa Bwana Nkurunziza alikuwa na virusi vya corona wakati anapata matibabu.

Serikali ya Burundi imeripoti visa 83 vya walioathirika na corona lakini pia hatua za Shirika la Afya Dunia za kukabiliana na virusi vya corona hazikuchukuliwa wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi huo.
Rais Pierre Nkurunziza

Pierre Nkurunzizaamekuwa mwanasiasa wa Burundi na kuwa madarakani tangu mwaka 2005.

Bwana Nkurunziza, kijana wa aliyekuwa mbunge, alinusurika mauaji 1993 ya wanafunzi wa Kihutu katika chuo kiuu cha Burundi ambapo alikuwa mhadhiri na kujiunga na waasi wa FDD kundi ambalo baadae lilibadilika na kuwa chama tawala cha CNDD-FDD ambacho alikuja akawa kiongozi.

Alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama rais wa Burundi.

Baada ya makubaliano ya Amani ya Arusha kati ya serikali na waasi, Nkurunziza alitajwa kuwa waziri wa mambo ya ndani kabla ya bunge kumchagua kama rais Agosti 2005.

2015, Nkurunziza alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na utata na chama chake kwa muhula wa tatu madarakani.

Wafuasi wake na wanaompinga Nkurunziza walikosa kukubaliana katika suala la ikiwa ilikuwa halali kwake kugombea tena na maandamano yakafuata.

Zaidi ya miezi miwili kulitokea maandamano ya kumpinga Nkurunziza ambayo yaliandamana na ghasia na kusababisha vifo vya watu.

Mei 13, 2015, jaribio la mapinduzi dhidi ya Nkurunziza lilitokea akiwa nje ya nchi hiyo.

Mkuu wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare alidai kwamba amemng'oa mamlakani Nkurunziza lakini wanajeshi watiifu kwa Nkurunziza walikanusha madai hayo.

Nkurunziza ameongoza taifa hilo kwa miaka 15.
Nkurunziza alipaswa kukabidhi madaraka

Rais Pierre Nkurunziza aliyezaliwa Desemba 18, 1963 alikuwa ameratibiwa kumkabidhi mrithi wake madaraka jenerali Evariste Ndayishimiye.

Burundi ndio tu imekamilisha uchaguzi mkuu mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi ya Burundi, katika uchaguzi uliofanyika Mei mwaka huu mgombea wa chama tawala cha Everiste Ndayishimye ndiye aliyetambuliwa kuibuka na ushindi.

hivyo basi, Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alitakiwa kumkabidhi madaraka.

Evariste Ndayishimiye, rais mteule amepangiwa kuapishwa Augosti 20 kumrithi Nkurunziza ambaye amekuwa akiongoza taifa hilo tangu 2005 yaani miaka 15.

Ndayishimiye ni mwanasiasa wa karibu wa Nkurunziza na amekuwa Katibu Mkuu wa Chama tawala cha CNDD-FDD tangu mwaka 2016.

Alizaliwa mwaka wa 1968 katika mkoa wa Gitega, eneo la kati mwa taifa hilo.
Siasa za Pierre Nkurunziza

Mwaka 2015, rais huyo aliyekuwa na miaka 51-aliyeingia madarakani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha mauaji ya watu 300,000, alisema kuwa hatawania tena nafasi hiyo ya urais kwa sababu ni kinyume na katiba.

Wafuasi wake walitetea kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2005 alichaguliwa na bunge na sio wapiga kura- na kutetea hoja hiyo katika mahakama ya katiba ya nchini humo.

Na kiongozi wa zamani wa waasi alimsifia kuwa kiongozi huyo ameleta amani katika utawala wake nchini Burundi.
Watu mashuhuri waanza kutuma risala za rambirambi

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambirambi na kufariji raia wa Burundi.

Pia rais Uhuru Kenyatta ametuma risala zake kwa familia ya Pierre Nkurunziza ambaye ameaga dunia.

Katika ujumbe wake, Rais Kenyatta amemtaja rais huyo aliyefariki kama mshirika mzuri katika kanda ambaye amehudumia nchi yake kama kiongozi wa taifa wa kipekee na kufanyakazi usiku na mchana akitafuta amani na uthabiti wa nchi yake na eneo la maziwa makuu kwa ujumla.

Rais amesema kuwa kifo kimepokonya kanda ya Afrika Mashariki kiongozi mashuhuri ambaye mchango wake katika kuunganisha kanda hii ni kitu kitakachokosekana na kumuomba Mungu kufariji familia, watu wa Burundi na eneo la Afrika Mashariki wakati huu wa maombolezi.

No comments: