Advertisements

Tuesday, October 27, 2020

EXAUD KIGAHE AAHIDI NEEMA JIMBO LA MUFINDI KASKAZIN

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe ametoa ahadi za neema wananchi wa jimbo hilo kama watampatia ridhaa ya kuwa mbunge wao.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe ametoa ahadi za nane kwa wananchi wa jimbo hilo kama watampatia ridhaa ya kuwa mbunge wao.
Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe ametoa ahadi za nane kwa wananchi wa jimbo hilo kama watampatia ridhaa ya kuwa mbunge wao.

Akizungumza wakati wa kufunga kamapeni za kuomba kura kwa wananchi wa jimbo la Mufindi,Exaud Kigahe alisema kuwa jimbo la Mufindi Kaskazini linakabiriwa na changamoto ya miundombinu ya Barabara ambazo zimekuwa hazipitiki kwa msimu mzima hivyo akipewa ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha anatatua kero hiyo.

Alisema kuwa atahakikisha anaboresha sekta ya Elimu kwa kujenga na kukarabati majengo ya shule,kuanzisha mashindano ya kumpata mwananfunzi bora na mwalimu bora kwa atakayefanya kazi nzuri ya kuwasaidia wanafunzi kufaulu kwa wastani mzuri.

“Wananchi wa jimbo la Mufindi wengi ni wakulima hivyo siwezi kuisahau sekta ya kilimo kwa kuwa hata mimi nimekulia kwenye family ya wakulima hivyo nitahakikisha kuwa tunaboresha masoko ya wakuliwa ili waweze kuuza mazao yao kwa bei nzuri” alisema Kigahe

Aidha Kigahe alisema kuwa ahadi nyingine ni pamoja na viwanda,afya,biashara,umeme na michezo ambazo atazifanyia kazi kama akiwa mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

“Kazi kubwa mliyonipa nitaifanya kwa nguvu na niwahakikishie sisi wabunge watatu wa Wilaya ya Mufindi (Kihenzile na Chumi) tutafanya kazi kwa pamoja kwa kuwa lengo kubwa ni kuleta maendeleo”alisema Kigahe

Kwa upende wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Dr Abel Nyamahanga ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi kwenye kufunga kampeni hizo aliwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuhakikisha wanampa kura nyingi Mgombea Ubunge Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe kwa kuwa ameamini na Rais.

No comments: