Na Deogratius Temba – Mbeya
Madiwani wanawake na maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka Halmashauri zaidi ya 20 nchini, wamefanya ziara ya mafunzo katika shule ya sekondari ya wasichana Galijembe katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Ziara hiyo ya kujifunza iliyofanyika leo Alhamisi,Novemba 19,2020 ni sehemu ya Tamasha la Jinsia la 6 ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), linalofanyika kuanzia Novemba 18 hadi 20,2020 katika Kijiji cha Hatuelo, kata ya Ijombe, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Viongozi hao walioambatana pia na baadhi ya wadau wa haki za wanawake na watoto, wametembelea shule hiyo maalumu ya wasichana ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, ambayo ilijengwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya halmashauri kwa kushirikiana na wananchi.
Ziara hiyo imelenga kuwapa fursa viongozi hao wa serikali za mitaa kujifunza ziadi jinsi ambavyo Halmashauri hiyo iliweza kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani, na kutenga fedha kwenye Bajeti yenye mrengo wa kijinsia ili kutatua changamoto za watoto wa kike katika kupata elimu.
Akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi, alisema kwamba uwepo wa shule hiyo ni sehemu ya mafanikio ya mafunzo mbalimbali ambayo madiwani, watendaji kata na Maafisa Mipango na Maendeleo ya Jamii walipatiwa na TGNP, ambapo walitenga bajeti kuhakikisha wanaboresha mazingira ya watoto wa kike kupata elimu.
“Tunaipongeza sana Halmashauri hii kwa jitihada za kuona umuhimu wa kutenga bajeti kwaajili ya kumsaidia mtoto wa kike ilia some vizuri. Sisi TGNP, tumejenga uwezo kwa wananchi kupitia uraghibishi, hatutoi fedha kwaajili ya kujenga miundombinu kama hii, lakini elimu tunayoitoa kupitia mafunzo kwa viongozi na jamii inasaidia sana kuhakikisha rasilimali wanazokusanya zinagawanywa na kutumika vizuri na kwa kuzingatia usawa kwa jinsi zote”, alisema Liundi na kuongeza:
“Kama kila Mtendaji wa Halmashauri anayepata mafunzo atasimamia vizuri rasilimali zetu na kuhakikisha tunapopanga bajeti tunazingatia mahitaji ya kijinsia tutakuwa na mafanikio makubwa sana, na kila mwananchi atafurahia na kunufaika na maendeleo yanayaopatikana”.
Awali akitoa maelezo juu ya ujenzi wa shule hiyo, ambayo tayari ina kidato cha kwanza na cha pili, iliyoanza mwaka 2019, Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri hiyo, Mwalingo Kisemba alisema kwamba, TGNP ina mchango mkubwa sana ambao ilisaidia viongozi na watendaji wa halmashauri hiyo kupata elimu na kuifanyia kazi.
“Sisi hapa kwetu baada ya kupata elimu kupitia mafunzo mbalimbali, tuliamua kuyatekeleza kwa vitendo. Tumetumia Zaidi ya asilimia 60 ya gharama za ujenzi wa shule hii kwa fedha za mapato ya ndani, fedha kidogo tulipewa kutoka serikali kuu na nyingine kwa wadau wetu wengine, lakini wananchi wa kata hii waliwajibika ipasanvyo. Niwaambie tu kwamba, kiongozi ukiamua kusimamia ukweli na ukawajibika vizuri utaona mafanikio na utakubalika na kila mmoja”, alisema Mwalingo
Madiwani wateule na watendaji wa Halmashauri waliofanya ziara hiyo ya mafunzo kuangalia mafanikio ya kutengwa kwa bajeti yenye mrengo wa kijinsia, wametoka katika halmashauri za Tarime, Kishapu, Moshi, Same, Muheza, Morogoro, Kilombero, Mvomero, Chamwino, Mtwara, Ilala, Pwani, Mbeya, Kalambo, Nkasi, Sumbawanga, Mbarali.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza wakati Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini walipotembelea Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza wakati Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini walipotembelea Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Mwalingo Kisemba ambaye ni Diwani Mteule wa kata ya Inyala akizungumza wakati Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini walipotembelea Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Galijembe, Anna Mwantengule akizungumza wakati Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini walipotembelea Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Nyanda za Juu, Denis Mwoleka akizungumza wakati Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini walipotembelea Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi (wa pili kulia) akiwa ameambatana na Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakiwa katika Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Muonekano wa majengo ya Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Muonekano wa majengo ya Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakiangalia majengo ya Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi,Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakiwa katika moja ya vyumba vya maabara ya Sayansi katika Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakiwa katika madarasa ya Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakiwa katika Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi (wa tatu kushoto), Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakitembelea Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Muonekano wa moja ya majengo katika Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Ziara ikiendelea katika Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Muonekano wa Bwalo la Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi, Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakiwa ndani ya bwalo la Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi,Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakiwa katika eneo la jiko katika Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi, Wadau wa haki za wanawake na watoto, Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakipiga picha ya kumbukumbu katika Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi, Wadau wa haki za wanawake na watoto, Madiwani wanawake na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka halmashauri mbalimbali nchini wakipiga picha ya kumbukumbu katika Shule ya Wasichana Galijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment