Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza akizungumza kwenye kikao cha Baraza kuu la CHADEMA lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewataka viongozi wa chama hicho kuacha kutumia mitandao kutoa maneno ya kudhalilisha na kuwatukana wanachama wa vyama vingine vya upinzani, badala yake amewataka waheshimu kutofautiana kwao.
Amewataka kuwa viongozi wa CHADEMA kuwa wanyenyekevu na kuheshimu mitazamo ya vyama vingine, pia wametakiwa kuacha tabia hiyo mara moja kwa kuwa tofauti ya kimtazamo ndio demokrasia yenyewe.
“Inaweza msipende maneno yangu lakini lazima niwaambie ukweli, nafasi ya chama chetu leo ni chama kikuu cha upinzani Nchini, haina maana nafasi hiyo tukawa nayo milele, yawezekana kesho ikawa chama kingine chochote,” - Mbowe
“Nchi yetu imejengwa kutoamiaminiana kwa miaka mingi, akionekana mpinzani ameenda Ikulu wanasema kuna biashara, mwingine akasema Mbowe amevuta bilioni 6 kwenda kumuona Rais, hayo ni mambo mepesi,” - Mbowe.
Katibu Mkuu wa Chama Mhe. John Mnyika akizungumza katika kikao cha Baraza Kuu la Chadema kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam Mei 11, 2022.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia kuhusu hali ya uchumi ambavyo sio nzuri na kuomba viongozi wa CHADEMA kushirikiana ili kuhakikisha hali ya uchumi inarudi vizuri katika kikao cha Baraza Kuu la Chadema kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam Mei 11, 2022.
No comments:
Post a Comment