Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa naibu makatibu wakuu wa wizara mbili na kuhamisha wengine watatu.
Taarifa iliyotolewa Jumatano Mei 11, 2022 na Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus imesema kuwa Rais Samia amemteua Dk Charles Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi (Elimu).
Dk Msonde amechukua nafasi ya Gerald Mweli ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo.
Kabla ya uteuzi huu Dk Msonde alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).
Dk Msonde ambaye ameiongoza Necta kwa miaka nane aliteuliwa kushika wadhifa huo Agosti 2014.
Dk Msonde aliteuliwa kushika wadhifa huo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Joyce Ndalichako aliyetangaza kuchukua likizo bila malipo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
No comments:
Post a Comment