Advertisements

Wednesday, January 20, 2021

Trump Amsamehe Aliyekuwa Mshauri Wake Dakika za Mwisho

RAIS anayeondoka madarakani, Donald Trump, amsamehe aliyekuwa mshauri wake, Steve Bannon, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya udanganyifu. Tangazo hilo linawadia saa kadhaa kabla ya kuapishwa kwa rais mteule, Joe Biden.

Trump pia amewasamehe watu wengine zaidi ya 140 saa zake za mwisho madarakani. Miongoni mwa waliosamehewa ni rapa Lil Wayne huku rapa mwingine Kodak Black na aliyekuwa meya wa Detroit, Kwame Kilpatrick, wakipunguziwa vifungo vyao.

Kwa ujumla watu 73 wamepewa msahamaha huku wengine 70 vifungo vyao vikipunguzwa, taarifa kutoka Ikulu ya Marekani imesema. Bannon, ambaye alikuwa mshauri mkuu wa Rais Trump wakati wa kampeni yake mwaka 2016, alipatikana na hatia mwaka jana kwa makosa ya udanganyifu juu ya kampeni ya kuchangisha pesa kuhusiana na kujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico.

Waendesha mashtaka, Bannon na wengine watatu, walidanganya mamia ya maelfu ya wafadhili kuhusiana na mradi wa kampeni ya “Tujenge Ukuta” ambayo ilikusanya dola milioni 25. Inadaiwa kuwa Bannon alipokea zaidi ya dola milioni 1 ambazo baadhi yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

Alikanusha makosa hayo na alikuwa ahukumiwe. Ikulu ya Marekani imesema Bannon amekuwa “Kiongozi muhimu na anajulikana kwa hekima yake katika siasa.” Taarifa hiyo ilisema kwamba waendesha mashtaka walikuwa wamemfungulia mashtaka yenye kuhusishwa na ulaghai kutokana na kujihusisha kwake kwenye mradi wa siasa
GPL

No comments: