ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 7, 2021

JHIKOMAN AWASHA MOTO NDANI YA ZANZIBAR RAGGAE FESTIVAL, ‘KUAGANA YABAMBA’


Jhikoman akiwa na bendi yake ya Afrikabisa wakitoa burudani kwenye onesho la kwanza la Zanzibar Reggae Festival, ndani ya Ngome Kongwe, Unguja, 6 Agosti, mwaka huu.


Na Andrew Chale, Zanzibar.

BENDI ya Afrikabisa yenye  maskani yake Bagamoyo, Pwani Tanzania, chini ya kiongozi wake Jhikolabwino Manyika maarufu Jhikoman imeweza kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa rege waliofurika kwa wingi kwenye tamasha la Zanzibar Reggae Festival, Ngome Kongwe.

 

Jhikoman ameweza kukonga nyoyo mashabiki hao ambapo alitumia zaidi ya saa moja jukwaani kwa kupiga nyimbo mbalimbali ikiwemo za zamani na za sasa ambazo zimeweza kufanya vizuri.

 

Miongoni mwa nyimbo alizopagawisha jukwaani ni pamoja na Afro Caribbean beat, Bad mind, Mpenzi, Ukipendwa, Moto,Mara ya kwanza na nyingine nyingi zikiwemo alizomuenzi msanii Bob Marley katika wimbo wa Hiden.

Wimbo wa Kuagana ambao alimalizia shoo yake hiyo, uliwezakushika hisia za mashabiki wa muziki wa rege waliofurika ambapo walitaka kurudiwa kwa wimbo huo.

 

Wapenzi wa muziki wa rege wakifurahia wakati wa shoo hiyo jana

Mashabiki wa muziki wa rege walionesha hali ya kufurahia muziki mzuri wa rege huku wakiomba Jhikoman arejee kwa mara nyingine siku ya mwisho ambayo ni usiku wa leo wa 7 Agosti.

 

Tara Jazz wakifanya yao jukwaa la Zanzibar Reggae Festival jana

Mbali na mwanamuziki Jhikoman na Afrikabisa, pia kundi la muziki wa kutoka Zanzibar la Tara jazz waliweza kutoa burundani ya aina yake ikiwemo ufundi wa hali ya juu ya kuchezea ala za muziki wa asili wa jazz wakichanganya vionjo vya muziki wa rege pia walikuwepo wasanii wengine wakiwemo Ras Jamaiel ambaye nae aliwasha moto kwenye jukwaa hilo.

 

Ras Kofi akitoa burudani katika jukwaa la Zanzibar Reggae Festival jana

Mwisho shoo hiyo ilifungwa na mwanamuziki Ras Kofi ambaye nae alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa rege waliofurika kwenye tamasha hilo siku ya kwanza.

Tamasha la rege Zanzibar msimu huu ni wa tatu tokea kuanzishwa kwake ambapo kila mwaka linakuja kitofauti ikiwemo wasanii wakubwa kutoka mataifa mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa tamasha hilo, Saidi Omary maarufu kama Saidi Side Rasta, alisema kuwa wasanii wakubwa na bendi  kutoka Mataifa zaidi ya 6 wamekuja kwa mara ya kwanza kutoa burudani ya muziki huo.

 


Nchi hizo ni pamoja na Jamaica, Ubelgiji, Marekani, na zingine ikiwemo Tanzania Bara na bendi za kutoka Zanzibar.

 

No comments: