ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 14, 2022

MBUNGE ALIA NA UBADHIRIFU WA MILIONI 588 JIMBONI KWAKE



Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hassan Mtenga amesema kumekuwepo na ubadhirifu wa Sh583 milioni zilizolipwa zaidi ya gharama halisi zilizokuwepo kwenye mkataba wa mkandarasi aliyepewa kazi ya kujenga taa za barabara jimboni humo.

Ameyasema hayo leo Alhamis Aprili 14, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2022/2023 bungeni jijini hapa.

Amesema jimbo lake lilikuwa na mradi wa kufunga taa barabrani 2017/2018, ambapo bajeti ya mkandarasi ni malipo ni Sh1 bilioni lakini Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na watumishi wengine walimlipa Sh1.65 bilioni.

Amesema kwa hiyo kuna Sh588 milioni zimelipwa nje ya mkataba na kwamba tayari Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alishasema fedha hizo zirudishwe.

Hata hivyo, Mtenga amesema fedha hizo hazijarudishwa hadi leo na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

No comments: