ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 25, 2022

TALIRI YATARAJIA KUTOA ELIMU YA MALISHO BORA MSOMERA





NA REBECA DUWE, TANGA

Taasisi ya utafiti wa mifugo iliyopo jijini Tanga yatarajia kutoa elimu ya malisho bora ya ng’ ombe kwa jamii ya wafugaji iliyotoka Ngorongoro na kuhamia Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dr. Zabron Nziku wakati akizungumza na waandishi wa ahabari Ofisini kwake hivi karibuni juu ya namna walivyojipanga kutoa elimu kwa wafugaji waliohamia Msomera kuwa na ufugaji boro wenye tija kwa maslahi yao na ya Taifa kwa ujumla.

Sambamba na hayo alisema wanatarajia kujenga kuwa na shamba la mfano la ufugaji wa Ng’ombe kupitia mradi wa ushirikiano na watu Ireland kwa ajili ya kuweza kuwasaidi wadau ambao ni wafugaji.

Aidha alisema wajibu wa taasisi hiyo ni kuwa saidia wafugaji hivyo kutokana wajibu huo wananchi waliotokea ngorongora ambao walikuwa wanafuga kienyeji watakuwa miongoni mwa wadau watakoweza kupata elimu ya ufagaji kwa kuweza kuwapa elimu malisho bora wa mifugo yao.

Dr. Nziku aliongeza kusema kuwa kwa kufanya hivyo serikali itaweza kupata mapato kupitia ufugaji boro wenye tija ambao utafanywa na watanzania hao endapo watachukua hatua ya kufanya kwa vitendo ufugaji huo.

No comments: