Na Timothy Itembe Mara.
Wanachama 29 ndani ya Chama cha mapinduzi wilaya Tarime ambao walichukua fomu za kugombea nyadhifa mbalimbali kwenye chama hicho wameishia mitini.
Akizungumza na mwaandishi wa habari ofisini kwake katibu wa CCM wilaya Tarime,Valentine Maganga alisema kuwa waliochukua fomu kugombea nafasi ya mwenyekiti ccm wilaya Tarime walikuwa 11 mwanamke mmoja na waliorudisha fomu walikuwa 10 mwanamke aliyechukua hakurudisha fomu,nafasi nyingine ni katibu siasa na uwenezi walichukua watu 8 wote wanaume na walirudisha watu 7,mkutano mkuu Taifa walichukua fomu 99 wanawake 8 ambao hawakurejesha ni watu 11.
Katibu huyo alitaja nafasi zingine kuwa ni wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa 39 wanawake 6 wasiorudisha fomu nafasi hiyo watu 3,halmashauri kuu ya wilaya waliochukua fomu ni watu 103 wanawake 16 wasiorejesha fomu watu 14 na kati ya wagombea nafasi hizo wapo watu wenye ulemavu 3 na wote walirejesha fomu.
Kwa upande wa katibu wa umoja wa vijana uvccm wilaya Tarime, Tito Paul Masele alisema kwenye jumuia yake hali ni shwari waliochukua fomu nafasi ya uwenyekiti ni watu 21 wanawake 2 waliorejesha ni watu 15 mwanamke 1,mjumbe 1 wa kuingia mkutano mkuu wa ccm mkoa waliochukiua fomu ni watu 3 mwanamke 1 na wamerejesha wote mwanamke ameishia mitini,mjumbe wa kuingia mkutano mkuu wa ccm wilaya nafasi moja na alichukua 1 na amerejesha huyo huyo,wajumbe watatu wa umoja wa vijana mkoa waliochukua fomu walikuwa watu 3 mwanamke 1,wajumbe 2 wabaraza la uvccm mkoa waliochukua fomu watu 14 walirejesha wanaume 5 wanawake 3,wajumbe 5wa uvccm wilaya walichukua 9 wanaume na wamerejesha 4mjumbe 1 kutoka uvccm wa kuwakilisha wazazi 1,mjumbe 1 kuwakilisha jumuia ya UWT nafasi ya upendeleo kwa wanawake walichukua 3 na amerejesha 1na kuwa kwenye jumuia hiyo waliochukua fomu niwagombea 63 wanawake 11 wanaume52.
Katibu huyo aliwataka wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi ndani ya chaka chake na kuwataka vijana kuchangamkia frusa pindi inapotokea kwasababu nafasi nichache kupatikiana.

No comments:
Post a Comment