ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 25, 2022

WAZIRI MKUU AITISHA KIKAO KUANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS SAMIA KUHUSU ENEO JIPYA LA MNARA WA MASHUJAA



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 25, 2022 ameitisha kikao cha kujadili utelekezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa jijini Dodoma la kuitaka Ofisi ya Waziri Mkuu itafute eneo jingine utakapojengwa mnara mpya wa mashujaa wenye hadhi ya Makao Makuu ya nchi.
Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akiongoza kikao hicho kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.

No comments: